Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sakata la Harmonize, Killy na Cheed ngoma nzito, Jumatano…

Muktasari:

Ule uamuzi wa kumalizana kati ya wasanii Ally Omar ’Killy’, Rashid Mganga ’Cheed’ na msanii Rajab Abdul ’Harmonize’ uliokuwa yafanyike leo Jumatatu, Oktoba 24, 2022 umeshindikana baada ya mwanasheria wa Harmonize kupata dharura na badala yake utafanyika Jumatano hii.

Dar es Salaam. Ule uamuzi wa kumalizana kati ya wasanii Ally Omar ’Killy’, Rashid Mganga ’Cheed’ na msanii Rajab Abdul ’Harmonize’ uliokuwa yafanyike leo Jumatatu, Oktoba 24, 2022 umeshindikana baada ya mwanasheria wa Harmonize kupata dharura na badala yake utafanyika Jumatano hii.

Wasanii hao leo Jumatatu Oktoba 24, 2022 ilikuwa wavunje mkataba rasmi kimaandishi mbele ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na lebo ya Konde Music Worldwide inayomilikiwa na Harmonize.

Basata ndio walikuwa wakisikiliza malalamiko yao ya kuvunjwa kwa mkataba huo bila ya kufuatwa kwa utaratibu pale lebo hiyo ilipotangaza kuachana nao Oktoba 10, 2022.

Baada ya kukaliwa kwa vikao viwili kwa siku tofauti, Baraza iliagiza lebo hiyo kwenda kutekeleza yale waliyobaliana kwenye mkataba endapo upande mmoja utauvunja na leo ndio ilikuwa watekeleza hilo kwa maandishi lakini ndio hivyo imeshindikana.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Ofisa Maendeleo Sanaa, Abel Ndaga amesema ni kweli ilikuwa wakamalizane leo lakini imeshindikana baada ya mwanasheria wa Harmonize kuomba udhuru kutokana na kutingwa na majukumu mengine na sasa watalifanya hilo Jumatano ya Oktoba 26, 2022.

“Kikao ilikuwa tukae saa sita mchana  tumalizane na jambo hili leo, lakini ndio hivyo, mwanasheria ambaye ni mtu muhimu pia katika kulishuhudia hili la kumalizana kwa wasanii hawa, amepata udhuru,” amesema Ndaga ambaye ndiye mwenyekiti wa vikao vyote vilivyofanyika katika sakata hilo tangu lilipoanza kusikilizwa Oktoba 12,2022.

Kwa upande wake, Meneja wa kina Cheed, Saty Sembe amesema wamekubaliana na uamuzi huo wakusogezwa mbele kwa siku na wana imani litakwisha salama.

Killy na Cheed waliojiunga rasmi na lebo hiyo Septemba 2020 wakitokea lebo ya King’s Music inayomilikiwa na msanii Ali kiba.

Kwa miaka miwili waliyokuwepo Konde Music, Killy aliweza kutoa nyimbo nne ikiwemo Mwisho, Vumilia, Roho na ‘Ni Wewe’ wimbo aliomshirikisha Harmonize na ambao ndio wimbo wake uliofanya vizuri kuliko zote tangu atue kwenye lebo hiyo na umeshatazamwa na zaidi ya mara milioni sita.

Ni Wewe ni wimbo uliotumia midundo ya wimbo wa Sina Makosa uliowahi kuimbwa na bendi ya Les Wanyika wimbo ambao pia uliwahi kurudiwa na Cool James mtoto wa Dandu.

Kwa upande wake Cheed akiwa konde alitoa nyimbo tatu ikiwemo Wandia, Final na Ndoa.