Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Teyana Taylor amshukuru Jay Z baada ya kutumbuiza naye

Muktasari:

  • Taylor alimshukuru Jay Z kwa imani, heshima na fursa aliyompa ya kuwa sehemu ya usiku huo wa kihistoria, akisema hawezi kuyachukulia poa matukio kama hayo na ataendelea kuyakumbuka maisha yake yote.

Marekani. Msanii wa Marekani, Teyana Taylor, amemshukuru gwiji wa Hip Hop nchini humo, Jay Z kwa kumpa nafasi ya kutumbuiza katika tamasha la kuadhimisha kumbukizi ya kuachiwa kwa albamu zake mbili za mwanzo.


Taylor alimshukuru Jay Z kwa imani, heshima na fursa aliyompa ya kuwa sehemu ya usiku huo wa kihistoria, akisema hawezi kuyachukulia poa matukio kama hayo na ataendelea kuyakumbuka maisha yake yote.


Mwimbaji huyo alikuwa miongoni mwa mastaa walioalikwa kutumbuiza katika show tatu za tukio hilo katika uwanja wa Yankee, ambapo show ya mwisho ilipewa jina la Extra Innings.


Tamasha hilo lilifanyika kwa siku tatu mfululizo kwa ajili ya kuadhimisha miaka 30 ya albamu ya Reasonable Doubt (1996), na miaka 25 ya albamu ya The Blueprint (2001), pamoja na show maalum ya ‘Extra Innings’ iliyoandaliwa kwa ajili ya mashabiki.


Jay Z, mkali wa kibao cha Young Forever (2009), alipata umaarufu kupitia albamu yake ya kwanza, Reasonable Doubt (1996) ambayo ilitoka chini ya chini ya Roc-A-Fella Records, huku ikikaa katika chati ya Billboard 200 kwa wiki 18.


Katika tamasha hilo, Taylor alifungua show kwa kuimba sehemu ya Mary J. Blige kwenye wimbo, Can’t Knock the Hustle (1996), uliopo kwenye albamu hiyo ya Jay Z.



Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Taylor ameeleza kuwa licha ya kukumbana na changamoto kadhaa akiwa jukwaani, bado anashukuru kwa nafasi hiyo hadhimu aliyopata.


Alieleza kuwa kusimama juu ya jukwaani hilo pamoja na Jay Z tena mbele ya mashabiki zaidi ya 40,000 uliojitokeza katika uwanja wa Yankee, ilikuwa ndoto ambayo hakuwahi kufikiria ingeweza kuja kutimia.


Taylor aliongeza kuwa tukio hilo limemkumbusha jinsi Mungu alivyoendelea kumwongoza na kumfikisha hatua kubwa katika maisha na kazi yake ya muziki.


Mbali na Teyana Taylor, wasanii wengine waliotumbuiza katika tamasha hilo ni pamoja na Beyonce, Rihanna, Usher, Fat Joe, Jadakiss, Pharrell Williams, Clipse, Alicia Keys, Eminem na Nas, ambao kwa pamoja waliinogesha hafla hiyo ya kihistoria.