Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ubora wa Prof. Jay 'unapozikwa na Audio'

Muktasari:

  • Zamani wimbo bora ulikuwa hauna video hapa Bongo. Kwa sababu ‘audio’ zilikuwa nzuri kuliko video. Waliamini video ni kuuharibu wimbo. Kwenye hili ni kweli walikuwa sahihi kwa sababu ‘kualite’ ya video ilikuwa ya kibwege.

Dar es Salaam, Jaribu kuwaza. Pini la Profesa Jay kama ‘Bongo Dar es Salaam’. Litupie kwenye video la dunia ya sasa. ‘Handsome’ ya Dully na ‘Bishoo’ ya Jaymoe? Achana na Staki Dem ya Juma Nature.

Zamani wimbo bora ulikuwa hauna video hapa Bongo. Kwa sababu ‘audio’ zilikuwa nzuri kuliko video. Waliamini video ni kuuharibu wimbo. Kwenye hili ni kweli walikuwa sahihi kwa sababu ‘kualite’ ya video ilikuwa ya kibwege.

Profesa Jay. Katika maisha yake kwenye muziki. Hakuna albamu yake bora kama  ‘Machozi Jasho na Damu’. Humo ngoma baada ya ngoma ni kali. Lakini hakuna ngoma hata moja yenye video. Inakera.

Pini kama ‘Bongo Dar es Salaam’. Ni nani angeitendea haki kwa video nyakati zile? Wangetuharibia pini la nchi. Ndivyo ilivyo kwa Jina Langu, Ndiyo Mzee, Tathmini, Nawakilisha, Piga Makofi na zilizobaki.

Tulikuwa bado. Hatukuwa na vifaa vya kisasa na watu sahihi wenye elimu na kazi hiyo. Wengi walifanya kwa mizuka na siyo taaluma. Ndicho kilichopo hata kwa Swahiba wake Sugu.

Mambo ya Fedha, Mikononi mwa Polisi, Chini ya 18. Zote hizo ni ngoma ambazo zilistahili kuishi katika video siyo audio. Lakini nani angefikia kiwango kile cha ‘prodaksheni’ ya Joakim Kimario? Nyie mnamuita Master Jay.

Nani angetendea haki mikono ya Majani katika goma la ‘Kama Unataka Dem’ ya Jaymoe, Solo Thang na Chillah? Mikono ya Bonny Luv katika ‘Mabinti’ ya Mwana Fa? Audio zilikuwa mbele ya muda kuliko video.

Sasa ni kinyume chake. Ukiwa makini bila pombe kichwani utagundua hili. Kwamba audio ni ‘loo kwalite’ mbele ya video za sasa. Yaani mavideo ya dunia hii ni unyama sana kuliko audio za kipindi hiki.

Leo huwezi kuona video za Kipaimara na Komonio kama siyo ‘kicheni pati’. Video zipo kwenye kilele cha ubora. Kama una video mbovu huwezi kutengeneza pesa kwenye ‘platforms’ za dunia hii. 

Na bahati nzuri ‘nau deizi’ huhitaji elimu wala makamera ya Adam Juma. Simu tu inatosha kukupa kitu bora na ukaishi tu. Teknolojia ipo juu sana kuliko uwezo wa akili zetu. Tunaachwa mbali sana na hizi teknolojia.

Muziki ni shamba lenye mavuno kuliko sanaa yoyote Bongo kwa sasa. Muziki una utajiri na ajira nyingi. Shilole leo hii anatengeneza pesa kupitia misosi, lakini chanzo ni muziki uliomfungulia milango zaidi.

Kwenye sanaa ya filamu hakupata kile alichopata kwenye muziki. Ni dhahiri kwa sasa muziki una malisho mazuri zaidi.

Alishtuka mapema kabla ya jua la jioni. Kina Wolper wako ‘bize’ na mengine kuliko filamu.

Katika mazingira haya ni ngumu Wema ‘kuinjoi’ kuitwa staa wa filamu. Lakini Shilole licha ya pesa za upishi, ni rahisi kwake ‘kuinjoi’ kuitwa staa wa muziki.

Wasanii wengi wa filamu ‘wanadili’ na madili mengine kwa sasa.

Mtu kama Kajala ni rahisi kumsikia kwa tukio la binti yake kuliko sanaa yake. Na Uwoya ‘anashaini’ na ulokole wake kuliko kile kilichompa ‘ustaa’. Hata tamthilia zinazokimbiza sasa hazina malisho bora kama muziki.

Biashara yoyote inapokubalika huwezi kuzuia ushindani wake. Katika muziki hali iko hivyo pia. Upo ushindani kwenye utunzi, shoo mpaka video. Ndiyo maana hupanda ndege kufuata ubora wa video ‘na ‘lokesheni’ kwingineko.

Lengo ni kutaka kuteka soko la kimataifa kwa video nzuri. Na wamefankiwa sana katika hili. Achana na midundo. Puuzia sauti hadi ‘melodi’. Weka kando ubora wa shairi. Video ya Number One ilimpa njia Diamond. 

Kupitia ubora wa video kama ile ilikuwa rahisi kumshawishi Davido akaelewa. Na ndiyo kilichotokea kwa Iyanya na wasanii wengine aliofanya nao kazi. Mbali ya hilo pia ikawa mfereji wa tuzo za kimataifa kwake.

Zamani Bongo Movie walipotuambia wana filamu ya kimataifa. Ujue ni filamu ambayo huwezi kuangalia na wazazi. Waliamini kimataifa ni uzungu uzungu kuanzia mavazi na viingereza vingi vya kunyapianyapia.

Kinachouma muziki kwa sasa hivi. Video zimechukua nafasi kiasi cha ubora wa mashairi kuwekwa kando. Yaani audio hazina ubora kuliko video. Kuna uvivu wa kuandika na ubunifu kimashairi. Wanajali zaidi video.

Inaumiza zaidi kuona kazi bora za Prof. Jay, zikiishi kwenye audio kuliko video. Nyimbo zilizostahili video kali kama za sasa, zilitoka muda ambao audio mbovu za sasa ndiyo zilizostahili video mbovu za zamani. Inakera.

Nyimbo nyingi za sasa zilipaswa kupewa video mbovu za zamani. Nyimbo nyingi za zamani zilipaswa kupewa video ‘klasiki’ kama za sasa. ‘Imejini’ pini kama ‘Mtoto wa Geti Kali’ lingepata video la dunia hii. Vipi pini kama Geto Langu la Ngwea?

Ndiyo Mzee haina video? Piga Makofi? Promota Anabip? Kikao cha Dharula? Okay, hata Chemsha Bongo? Mamsapu? Hizi kazi bora zaidi za muziki wa kizazi kipya za The Heavy Weight Mc Prof. Jay zisizo na video.