Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uhusika wangu wa Jonasi unaniletea shida

Muktasari:

  • Akizungumza katika mahojiano na TimesLIVE, Mtshali alisema watu wengi wameshindwa kutofautisha kati ya S'dumo na Jonasi, jambo ambalo limekuwa changamoto katika maisha yake binafsi.

Afrika Kusini. Mwigizaji kutoka Afrika Kusini, S'dumo Mtshali, amesema uhusika wake wa Jonasi Gomora katika tamthilia ya The Polygamist umemfanya kuwa mmoja wa waigizaji wanaozungumziwa zaidi, huku baadhi ya watazamaji wakimchukia hadi katika maisha yake halisi.


Akizungumza katika mahojiano na TimesLIVE, Mtshali alisema watu wengi wameshindwa kutofautisha kati ya S'dumo na Jonasi, jambo ambalo limekuwa changamoto katika maisha yake binafsi.



"Nimegundua watu wengi wanamzungumzia Jonasi kuliko hata S'dumo. Wengine wakiniona huonyesha hasira kutokana na matendo ya Jonasi, jambo linalonifanya nijue nimeucheza vizuri uhusika huo," amesema.


Katika tamthilia hiyo, Jonasi ni mfanyabiashara mwenye mafanikio ambaye kwa nje anaonekana kuwa mume na baba wa mfano. Hata hivyo, nyuma ya pazia anaishi maisha ya udanganyifu, usaliti na mahusiano ya siri yanayosababisha migogoro mikubwa ndani ya familia yake.


Mtshali amesema lengo la tamthilia hiyo halikuwa kuwaburudisha watazamaji pekee, bali pia kuwaelimisha na kuwafanya wafikirie kuhusu matatizo yanayotokea katika familia nyingi. Kwa upande wake, anaamini matendo ya Jonasi yanatokea katika maisha halisi kupitia ndugu, jamaa au marafiki, ndiyo maana tamthilia hiyo imepata mwitikio mkubwa.


Mwigizaji huyo amesema kuuvaa uhusika wa Jonasi haikuwa kazi rahisi. Alilazimika kuingia kwa undani katika tabia na fikra za mhusika ili aonekane wa kweli mbele ya watazamaji. Kutokana na uzito wa uhusika huo, amesema hata wazazi wake walikuwa wakimwombea wakati wote wa kurekodi tamthilia hiyo.


Aidha, amesema wakati wa maandalizi ya kurekodi tamthilia hiyo alifuatilia matukio na watu wenye tabia zinazofanana na za Jonasi, jambo lililomsaidia kuuvaa vyema uhusika huo.



Mtshali pia alifichua kuwa riwaya ambayo tamthilia hiyo imetokana nayo ina matukio makali zaidi kuliko yale yaliyoonyeshwa kwenye tamthilia, lakini watayarishaji waliamua kupunguza baadhi ya sehemu ili simulizi liendelee kubeba ujumbe wake bila kuzidisha ukatili.


Kwa upande wake, mwandishi wa riwaya hiyo, Sue Nyathi, amesema amefurahishwa kuona tamthilia hiyo imezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii. Amesema lengo lake lilikuwa kuanzisha mazungumzo kuhusu masuala ya ndoa, mahusiano na nafasi ya mwanaume katika familia.


Tangu kuanza kuonyeshwa kwenye Netflix, The Polygamist imeendelea kufanya vizuri katika nchi mbalimbali za Afrika, huku Jonasi Gomora akiendelea kuwa mmoja wa wahusika wanaozungumziwa zaidi kutokana na matendo yake ndani ya tamthilia hiyo.