Uwoya, Mbosso wazua utata

Muktasari:
- Wawili hao kuna muda wamekuwa wakionekana baadhi ya sehemu mbalimbali wakiwa pamoja na hata Uwoya kupenda kuposti picha ya nyota huyo anayetamba na ngoma ya Aviola na kuandika maneno ya upendo.
Dar es Salaam. Hivi karibuni Irene Uwoya na Mbosso wameonekana kuwa karibu sana na kuzua utata kwa mashabiki zao.

Wawili hao kuna muda wamekuwa wakionekana baadhi ya sehemu mbalimbali wakiwa pamoja na hata Uwoya kupenda kuposti picha ya nyota huyo anayetamba na ngoma ya Aviola na kuandika maneno ya upendo.
Mashabiki zao wamestushwa na ukaribu huo na kuzua utata wa kujipa majibu tofauti tofauti ya kidai huenda wanaweza kuwa na ukaribu wa kawaida ama wa kimahusiano.
Mwananchi lilipiga stori na Uwoya na kufafanua, yeye na Mbosso ni marafiki wa muda mrefu ila watu wamechelewa kufahamu.

“Kitu ambacho watu wengi hawakijui mimi na Mbosso ni marafiki wa muda mrefu na kila mmoja ni shabiki wa mwenzake kupitia kazi zetu, hakuna kitu kingine na hakitawahi kutokea,” alisema Uwoya.
Kwa upande wa Mbosso, alisema; “Kwanza nashukuru sana kupata rafiki mwenye upendo wa dhati, Irene Uwoya ni dada mwenye upendo sana, Mungu azidi kumbariki, watu wasiwe na fikra tofauti tu mara wanapoona jinsia tofauti zipo karibu, hakuna cha mapenzi wala nini, sisi ni marafiki tena tumekuwa kama ndugu sasa.”
Oktoba 3, 2025, ikiwa ni kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Mbosso, post ya mwigizaji Irene Uwoya akimtakia kheri ya kuzaliwa msanii huyo ilizua gumzo. Post yake liliyoambatana na picha yao wakiwa pamoja.