Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gawio la Serikali laongezeka hadi Sh1.8 trilioni

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu.

Muktasari:

  • Gawio hili kwa mwaka huu limeongezeka kwa asilimia 30 kutoka lile lililotolewa na taasisi na mashirika ya umma mwaka jana.

Dar es Salaam. Serikali imekusanya jumla ya Sh1.32 trilioni hadi jana Jumatatu, Juni 29, mwaka huu, ikiwa ni gawio na michango mingine kutoka mashirika na taasisi ambazo inamiliki hisa chache.

Kiwango hicho cha makusanyo ni ongezeko la Sh300 bilioni, sawa na asilimia 30, kutoka Sh1.02 trilioni kilichokusanywa Juni mwaka jana.

Hayo yameelezwa leo, Jumanne Juni 30, 2026 na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu alipozungumza katika hafla ya siku ya gawio, ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ni mgeni rasmi, Ikulu ya Dar es Salaam.

“Kama tungekuwa tunahesabu fedha zote zinazotoka kutoka taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, kiasi hiki kingekuwa kikubwa zaidi,” amesema.

Amesema mwaka huu hawakuhesabu mapato ya taasisi nne ambazo ni Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (Sh70.7 bilioni) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (Sh114.14 bilioni), Shirika la Hifadhi za Taifa (Sh208.5 bilioni) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Sh90.39 bilioni.

Mchechu, amesema iwapo viwango vyote vya fedha vingekusanywa na kurekodiwa, jumla la gawio lingefika Sh1.811 trilioni.

Katika mkakati waliojiwekea na Wizara ya Fedha na ukuaji uliopo, amesema lengo la kutaka mapato yasiyo ya kikodi yafikie asilimia 10 kabla ya 2030 yatafikia kabla ya mwaka huo.

Amesema hilo inachangiwa na umahiri, usimamizi wa maelekezo, umakini wa bodi na uongozi wa taasisi.


Endelea kufuatilia Mwananchi