Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kenya kuzitoza ushuru bidhaa za Tanzania, Uganda

Katibu mkuu wa Wizara ya Biashara Kenya, Chris Kiptoo

Muktasari:

  • Tanzania na Uganda wanayo orodha ya bidhaa wanazozishuku kutokidhi vigezo vya asili ya bidhaa

Dar es Salaam. Baada ya mvutano wa miezi kadhaa ya bidhaa zake kutozwa ushuru mkubwa tofauti na mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Kenya imesema itaanza kufanya hivyo kwa bidhaa za Tanzania na Uganda kuanzia Julai Mosi.

Kuanzia Machi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na ile Uganda (URA) zimekuwa zikizitoza ushuru wa asilimia 25 bidhaa tamu kutoka Kenya kama vile pipi, chokuleti, juisi na ice cream.

Katibu mkuu wa Wizara ya Biashara Kenya, Chris Kiptoo alisema baada ya mazungumzo yaliyofanyika kati ya pande husika ndani ya kipindi cha mgogoro huo, Serikali imetoa mwezi mmoja zaidi na endapo hakutakuwa na mabadiliko, kuanzia Julai, Kenya pia itaanza kuzitoza ushuru huo bidhaa za Tanzania na Uganda.

Katibu mkuu huyo alisema timu za wataalamu watakaothibitisha kama bidhaa hizo zinatumia sukari ya viwandani iliyosamehewa kodi kutoka Tanzania na Uganda zitaingia nchini humo kuanzia Juni 11 ili kujiridhisha.

“Tunafanya uamuzi baada ya uthibitisho kufanyika. Ikibidi tutalipiza kisasi lakini lazima tujipe muda kabla ya kufanya hivyo. Tutafanya uamuzi huo Juni 30,” alisema Kiptoo.

Mchakato huo wa kuthibitisha malighafi inayotumika kutengeneza bidhaa zinazolalamikiwa utasimamiwa na sekretarieti ya EAC na kuhusisha viwanda vya bidhaa nyingine kama vile saruji, vilainishi vya mitambo, vipodozi na bidhaa za mbao ambazo mara nyingi zimekuwa zikipata vikwazo kuingia Tanzania.

“Tanzania na Uganda wanayo orodha ya bidhaa wanazozishuku kutokidhi vigezo vya asili ya bidhaa (certificates of origin), hivyo kuzitoza ushuru kinyume na mkataba wa biashara huru wa EAC wa mwaka 2010,” alisema Kiptoo.

Tangazo hilo lilitoa msamaha huo kuanzia tarehe ya kutolewa kwake hadi Julai 31, 2017 likiruhusu kuingiza tani 9,000 za maziwa ya unga na sukari isiyo na kikomo.