Master J apata mtoto

Friday April 02 2021
mastarjapic
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, Master J  na mpenzi wake Saraha Kahisi maarufu Shaa ambaye ni msanii wa Bongofleva wamepata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa mtayarishaji huyo.

Master J alitangaza ujio wa mtoto hiyo  katika mtandao wa kijamii wa Instagram leo Ijumaa Aprili 2, 2021 huku akiweka picha ya Shaa aliyewahi kutamba na kundi la Wakilisha lililokuwa likiundwa na wasanii wengine wawili, Witness na Langa (marehemu).

Akizungumza na Mwananchi Digital, Master J aliyewasaidia wasanii wengi wanaotamba kwa sasa amesema ana watoto wengine watatu wa kike akibainisha kuwa wa kwanza na miaka 22, wa pili 19 na watatu 16.

“Mtoto huyu kapishana sana umri na ndugu zake wengine huenda baadaye wakaja kuwa walezi wake..., ndio hivyo kama nilivyokuambia mtoto wangu wa mwisho ana miaka 16, hivyo ni wazi kuwa huyu kapishana kwa mbali sana na ndugu zake, lakini kwangu mimi ni burudani kwa kuwa huenda wakaja kumlea baadaye,” amesema.


Advertisement