Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maziwa yakosa soko Mbeya

Muktasari:

  • Mbeya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imesema inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa soko la maziwa na viwanda vya kusindika licha ya wafugaji kuzalisha lita 54 milioni kwa mwaka.

Mbeya. Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imesema inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa soko la maziwa na viwanda vya kusindika, licha ya wafugaji kuzalisha lita 54 milioni kwa mwaka.

 Ofisa Kilimo na Mifugo Wilaya ya Rungwe, Juma Mzara amesema leo Ijumaa, Agosti 4, 2023 wakati akizungumza na Mwananchi Digital, kwenye banda la maonyesho ya wakulima nanenane, katika viwanja vya John Mwakangale Jijini hapa.

Amesema kuwa wafugaji wamekuwa wakizalisha maziwa yenye ubora wa kiwango cha hali ya juu lakini ukosefu wa masoko na viwanda vya kusindika ni changamoto kubwa.

“Kwa sasa kwenye wilaya yetu tuna mnunuzi mmoja ambaye ni kampuni ya Asasi, huyu kujenga kiwanda ambaye amejenga kiwanda na kuwa kimbikilio japo bado kiasi kikubwa cha maziwa kinakosa soko,” amesema.

Mzara amesema kutokana na hali hiyo wafugaji wanalazimika kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya hasara ili kupata fedha kwa ajili ya kununua chakula cha mifugo hususan mashudu na madawa ya chanjo na kujikuta wakitumia gharama kubwa huku faida ikiwa ni ndogo.

“Tunaomba wawekezaji nchini kutumia fursa hiyo kwani maeneo yamehainishwa ikiwepo mapori yasiyo endelezwa, lengo ni kuwepo kwa uwekezaji wa viwanda vidogo na vya kati,” amesema.

Aidha Mzara ameomba Serikali kufanya jitihada za kushawishi uwekezaji kwenye sekta hizo kupitia maonyesho ya wakulima ambayo yanakutanisha wadau kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Mtendaji wa Chama cha Ushiriki wa Wakulima Wilaya ya Rungwe, Zawadi Mapunda, ameomba Wizara ya Mifugo kuona namna bora ya kutoa vifaa vya kipima joto la maziwa ili kubaini ubora kabla ya kuingizwa sokoni.

Amesema kuwa idadi kubwa ya wakulima wamekuwa wakiingiza sokoni bidhaa hiyo pasipo kupima ubora wake, na kwamba jambo hilo linatokana na gharama za vifaa hivyo.

“Uzalishaji wa maziwa kwa Wilaya ya Rungwe ni mkubwa huku kukiwa na kiwanda kimoja cha Kampuni ya Asasi, ndio tegemeo kubwa; tunaomba Serikali kulitazama suala hilo ili kusaidia wakulima na wafugaji kunufaika,” amesema.

Mfugaji Joel Mwakitalima amesema kuwa kutokana na changamoto ya masoko wanalazimika kuuza lita moja ya maziwa kati ya Sh700 mpaka Sh900 badala ya kuuza lita moja ya maziwa kwa Sh1,000 bei ambayo anadhani inaweza kuwanufaisha wafugaji wilayani humo.