Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchanga lori moja wanunuliwa kwa Sh1.2 milioni Manyara, Takukuru yashtuka

Vijana wakipakia mchanga kwenye lori. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoani Manyara imeingilia kati na kuokoa fedha za mradi wa ujenzi wa madarasa matatu na vyoo vya shule ya msingi Namalulu wilayani Simanjiro

Babati. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Manyara imeokoa fedha za mradi wa ujenzi wa madarasa matatu na vyoo katika Shule ya Msingi Namalulu wilayani Simanjiro, baada ya kubaini ubadhirifu uliofanywa katika ununuzi wa vifaa vya ujenzi.

Naibu Mkuu wa Takukuru mkoani Manyara, Anthony Gang'olo ameeleza hayo mjini Babati Mei 26, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Gang'olo amesema mradi huo wa ujenzi wa vyoo vya Shule ya Msingi Namalulu umebainika baada ya kufuatilia gharama za ujenzi wake na kusababisha kuokoa Sh2.05 milioni.

Amesema Ofisa Mtendaji wa Kiijiji cha Namalulu alinunua lori moja ya mchanga kwa Sh1.2 milioni wakati thamani halisi ya soko ilikuwa Sh450,000 pekee, hali ambayo iliyoisababishia Serikali hasara ya Sh750,000.

Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Manyara, Anthony Gang’olo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa taasisi hiyo.

Ameeleza kwamba ilibainika kuwa lori mbili za kokoto zilinunuliwa kwa Sh2 milioni badala ya bei halisi ya soko ya Sh1.225 milioni jambo lililosababisha hasara ya Sh775,000.

"Hata hivyo, makisio yasiyo sahihi ya mbao za upauzi wa mradi huo yalisababisha mbao 45 kubaki bila matumizi, hali iliyosababisha hasara ya Sh525,000 kwa serikali," amesema.

Ametoa wito kwa watumishi wa umma kutojihusisha na ubadhirifu pindi wakipatiwa dhamana ya kuongoza ofisi za Serikali kwani wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Mkazi wa Mtaa wa Nyunguu mjini Babati, Rose Tluway amepongeza juhudi zinazofanywa na Takukuru katika kuhakikisha wanawasimamia watumishi wabadhirifu.

"Pamoja na hayo inapaswa sheria kuwa kali zaidi ili kuwafanya watumishi wa umma kuogopa kufanya ubadhirifu wa fedha za umma," amesema Tluway.

Amesema endapo watumishi wa umma ambao ni wabadhirifu wakiwekewa sheria ngumu na zakuwabana watakuwa na hofu ya ufujaji wa fedha.