Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Puma Energy yazindua kituo cha kwanza cha gesi asilia (CNG) nchini Tanzania

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,   Felchesmi Mramba akikata utepe katika uzinduzi wa kituo cha Gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) Puma Energies kando ya Barabara ya Bagamoyo Tangibovu Mbezi Beach alipokuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. Pamoja naye kutokea kushoto ni Kaimu Balozi wa Canada nchini Tanzania, Carol Mundle,  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Puma Energies Tanzania, George Madafa, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah, Mkurugenzi mstaafu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni hiyo, Dk Selemani Majige. Na Mpigapicha Wetu

Kampuni ya Puma Energy imeweka historia mpya nchini Tanzania kwa kuzindua kituo cha kwanza cha rejareja cha gesi asilia iliyoshindikizwa (CNG), kilichopo Tangi Bovu, Barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam.

Hatua hii inadhihirisha dhamira ya kampuni hiyo ya kuendeleza nishati safi na suluhu bunifu za kimazingira.

Kituo hicho, kilichojengwa kwa viwango vya kimataifa, kina uwezo wa kusambaza futi milioni za ujazo wa gesi kwa siku na kuhudumia magari madogo, bajaji na malori makubwa ya mizigo. Kikiwa na mashine  mbili zenye kasi kubwa zinazoweza kuhudumia magari 50 kwa saa, kituo hiki pia kimeunganishwa na   na mashine ya kukandamiza gesi (compressor) kutoka Canada yenye uwezo wa kusukuma gesi zaidi ya mita za ujazo 1,200 kwa saa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania,  Fatma Abdallah amesema kituo hicho kinatoa huduma za CNG sambamba na bidhaa nyingine za Puma Energy kama petroli, dizeli, LPG, vilainishi na duka la huduma mbalimbali.

Amebainisha kuwa ni sehemu ya mkakati wa kampuni kupunguza uzalishaji wa kaboni na kuongeza urahisi kwa wateja, huku akithibitisha kuwa vituo zaidi vya CNG vitafunguliwa kabla ya mwaka huu kuisha.

Amesema kituo hicho pia kina hifadhi ya gesi ya lita 4,000 ili kuhakikisha inapatikana hata wakati wa mahitaji makubwa.

Amefafanua kuwa pia kimewekwa  mfumo madhubuti wa usalama na ukaguzi wa ubora ili kulinda wateja na kuhakikisha ufanisi.

“Kwa uwekezaji huu, Puma Energy inaendelea kuwa kinara katika kukuza upatikanaji wa nishati nafuu na safi, sambamba na kusaidia ajenda ya Serikali ya matumizi ya nishati yanayozingatia ulinzi wa mazingira.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, mhandisi Felchesmi Mramba, na wageni waalikwa wengine wakiwemo viongozi waandamizi wa Puma Energy pamoja na wawakilishi wa ubalozi wa Canada.