Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu ongezeko la watu kuwekeza masoko ya mitaji zatajwa

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA), Nicodemus Mkama, akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kuorodheshwa kwa hatifungani ya  kampuni ya iTrust Finance, kwenye soko la hisa la Dar es Salaam (DSE).

Dar es Salaam. Mazingira wezeshi na shirikishi yanayotolewa na serikali, yameelezwa kuwa ni moja ya sababu ya ongezeko la watu kuwekeza katika  masoko ya mitaji na dhamana hapa nchini.

Hayo yalisemwa jana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama kwenye hafla ya kuorodheshwa kwa hatifungani ya  kampuni ya iTrust Finance, kwenye soko la hisa la Dar es Salaam (DSE).

Mkama alisema licha ya kuwa imeingia kwa mara ya kwanza katika soko la hisa, iTrust wameweza kuvuka malengo na kuzidi kiasi cha programu kwa kuuza hisa zenye thamani ya Sh100 bilioni katika toleo la kwanza huku asilimia 98 ya wawekezaji wake wakiwa ni watanzania na asilimia 1.28 ndio wageni.

“Pia katika manunuzi hayo asilimia 66 ni wawekezaji mmoja mmoja na asilimia 33 ni taasisi  na kampuni,” ana sema.

Akifafanua zaidi, alisema hatifungani  hizo ambazo zilipaswa kuuzwa kwa awamu nne ndani ya miaka minne (yaani hadi mwaka 2029) hatua inayoonyesha ni kwa namna gani watu wamekuwa na imani na soko la mitaji hapa nchini.

“Ilikuwa ni programu iliyoidhinishwa na mamlaka kutolewa katika programu nne ambapo kwa awamu ya kwanza ilikuwa zitiliwe hati fungani  zenye thamani ya  Sh15 bilioni (2026), Sh30 bilioni (2027), Sh20 bilioni (2028) na Sh35 bilioni(2029), lakini katika toleo la kwanza tu wameweza kuvunja historia ya kuuza kiasi chote,” anasema Ofisa Mtendaji huyo.

Alisema mauzo ya hatifungani yamepata mafanikio ya saba zaidi ambapo kiasi cha Sh114.12 kimepatikana ikilinganishwa na Sh15 bilioni zilizotarajiwa kupatikana.

Kutokana na hilo anasema yanaifanya kampuni hiyo kuweka historia ya kuwa na mafanikio makubwa ya hatifungani kupita zote ambazo zilishawahi kutolewa hapa nchini.

“Hatifungani iliyokuwa inashikilia rekodi kubwa ni hatifungani ya Makazi Bond, ambayo ilipata  na mafanikio ya asilimia 661.1 na iliorodheshwa kwenye soko la hisa Juni 2026,” alisema Mkama.

Alisema mamlaka imefurahishwa kwa hatua hiyo na kutoa pongezi kwa kampuni na wataalamu waliohisika katika kuweka rekodi hizo katika masoko ya mitaji na sekta ya fedha hapa nchini.

Pia ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa sekta binafsi na watu wengine kuweza kutumia fursa zinazopatikana katika masoko ya mitaji ili waweze kupata rasilimali fedha zitakazotumika katika kukuza biashara na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande wa Ofisa Mwandamizi wa kitengo cha ushauri na Utafiti wa iTrust Finance, Samari Shirima, anasema uwekezaji huo unaenda kuwasaidia kuongeza mtaji kwa taasisi yao kufanya maboresho kwenye masuala ya kidigitali na kuwafikia.

Pia katika utekelezaji wa dira 2050, Shirima alisema kupitia maboresho hayo ya kidigitali wanaenda  kuwavutia  wawekezaji  na kuweza  kuwaleta watanzania wengi zaidi kwenye masoko ya hisa na mitaji.

“Pia kampuni zinaweza kupata mitaji ya kuendeleza biashara zao kwa kuwasaidia kutengeneza faidi zaidi na hatimaye kuchangia kuongeza kodi kubwa na kusaidia taifa kusukuma mbele mipango ya maendeleo.”

Mtendaji Mkuu wa iTrust Finance, Faiz Arab, alihusisha mwitikio huo mkubwa na imani ya wawekezaji katika mtindo wa biashara wa kampuni hiyo pamoja na fursa zinazozidi kupanuka katika soko la mitaji nchini.

Anasema wawekezaji wa kawaida (retail investors) walichangia asilimia 67 ya maombi yote ya uwekezaji, huku mifumo ya kidijitali ikiwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya ofa hiyo.

Kwa mujibu wa Arab, asilimia 58 ya maombi yenye thamani ya Sh66 bilioni yaliwasilishwa kupitia majukwaa ya kidijitali, huku programu ya iTrust App pekee ikichangia Sh54 bilioni, sawa na asilimia 47 ya maombi yote.

Fedha zitakazopatikana kupitia hati fungani hiyo ya miaka minne, yenye riba ya asilimia 13 kwa mwaka inayolipwa kila baada ya miezi mitatu, zitatumika kupanua majukwaa ya kidijitali ya kampuni, kuimarisha biashara ya mikopo inayotolewa kwa dhamana ya hati za uwekezaji na kuongeza huduma zake za kifedha.