Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali, sekta binafsi zatakiwa kushirikiana

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Omari Issa akizungumza na viongozi wa kampuni za biashara wa nchi mbalimbali, wakati wakijadili fursa za biashara nchini jijini Dar es Salaam jana. Picha na Anthony Siame

Muktasari:

Ni katika mkutano wa viongozi wa biashara wa nchi mbalimbali uliofanyika Dar es Salaam kujadili fursa za biashara.

Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais Utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Omari Issa amesema kuna umuhimu wa kuongeza ushirikiano baina ya Serikali na sekta binafsi ili kukuza kampuni kubwa zenye ufanisi.

Issa amesema kampuni hizo zitasaidia kutoa ajira na kuleta maendeleo nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa biashara kutoka nchi mbalimbali uliofanyika jana, jijini hapa, Issa alisema ushirikiano huo utapunguza mashirika ya umma kutegemea ruzuku Serikalini.

Issa alitoa mfano kuwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuwa linaendeshwa ‘kifamilia’ chini ya mwamvuli wa taifa unaolifa liwekewe mazingira ya kubaki mikononi mwa Serikali badala ya kuharakisha mchakato wa kushirikiana na sekta binafsi.

“Lazima tuanze kubadilika na kufikiri kibiashara. Hata Air Tanzania tukikubaliana tuingie ubia na watu wengine, tuingie tufanye biashara. Tuiruhusu iende hivyo lakini tusitegemee kila siku ruzuku ya Serikali, hatutafika,” alisema.

Katika mkutano huo, sekta za kilimo na utalii zilitajwa kuwa miongoni mwa vinara wa zile zinazolipa haraka na kwa kiwango kikubwa kwa sasa, iwapo wawekezaji wa ndani na nje watawekeza vilivyo mitaji yao.

Kwa mujibu wa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia (WB) nchini, Yutaka Yoshino, kilimo ni sekta inayoweza kuwa na faida kubwa iwapo itafanywa kibiashara.

Yoshino alisema hadi sasa Tanzania haijafanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwa na uwekezaji mkubwa wa kilimo unaofanywa kisasa, hivyo iwapo wawekezaji watawekeza fedha watapata faida kubwa na haraka.

“Pamoja na sekta hiyo kulipa, kuna tatizo kubwa la kupata ardhi. Mchakato wa kupata eneo ni mgumu sana unaohusisha taratibu lukuki za kukatisha tamaa,” alisema Yoshino wakati akijibu swali la Andrew Hart ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Afex kutoka nchini Kenya.

Mtaalamu huyo alisema siku za hivi karibuni kilimo kimeanza kukua, hasa baada ya muda mrefu kukua chini ya asilimia nne na kushindwa kusaidia kutoa ajira ipasavyo, licha ya kuwa zaidi ya asilimia 85 ya Watanzania wanaitegemea sekta hiyo.

Yoshino alisema kwa mtazamo wake, utalii ni sekta ya pili yenye maslahi zaidi kutokana na fursa mbalimbali kuendelea kufunguliwa.

Alisema mbali na kuwepo fursa katika maeneo yaliyozoeleka ya Zanzibar na Kanda ya Kaskazini, Serikali inazidi kuhamasisha na kufungua milango zaidi ya kuwekeza kupitia sekta hiyo katika Kanda ya Kusini.

Huku akitumia baadhi ya takwimu za kiuchumi, mtaalamu huyo alisema Kanda ya Kaskazini ina thamani kubwa lakini fursa zake hazitumiki ipasavyo.