Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sotta Mining kufungua fursa za ajira Tanzania

Muktasari:

  • Wadau wa sekta ya madini, serikali, sekta binafsi na asasi mbalimbali wamekutana jijini Mwanza kujadili utekelezaji wa sera za maudhui ya ndani.

Mwanza. Mradi wa Dhahabu wa Nyanzaga unaosimamiwa na kampuni ya Sotta Mining Corporation Limited umesema mafanikio ya mradi hayapimwi kwa kiwango cha dhahabu kitakachozalishwa pekee, bali kwa mchango wake katika maendeleo ya wananchi na uchumi wa Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Sotta Mining Corporation nchini, Isaac Lupokela katika Kongamano la 5 la Uzingatiaji wa Maudhui ya Ndani (Local Content Compliance Forum – LCCF) lililoanza leo Jumatano, Julai 22-24, 2026 jijini Mwanza.

Kongamano hilo limewakutanisha wadau wa sekta ya madini, serikali, sekta binafsi na asasi mbalimbali kujadili utekelezaji wa sera za maudhui ya ndani.

Ushiriki wa Sotta Mining katika kongamano hilo unakuja wakati ambapo Mradi wa Nyanzaga unatajwa kuwa mgodi mkubwa wa kwanza wa dhahabu unaotarajiwa kuanza uzalishaji mapema mwaka 2027.

Mgodi wa Nyanzaga unatekelezwa na Sotta Mining Corporation Limited, kampuni ya ubia inayomilikiwa kwa asilimia 80 na Perseus Mining na asilimia 20 na Serikali ya Tanzania.

Muundo huo wa umiliki unalenga kuhakikisha taifa linashiriki moja kwa moja katika thamani ya kiuchumi inayozalishwa na mradi huo, ambao unatarajiwa kuanza uzalishaji wa kibiashara katika robo ya kwanza ya mwaka 2027.

Lupokela, amesema mafanikio ya mradi hayapimwi kwa kiwango cha dhahabu kitakachozalishwa pekee, bali pia kwa mchango wake katika maendeleo ya wananchi na uchumi wa Tanzania.

"Ushiriki wetu katika kongamano la uzingatiaji wa maudhui ya ndani unaakisi dhamira yetu ya kuhakikisha mradi wa Nyanzaga unakuwa ushirikiano wa kweli na Tanzania.

Huu ni mgodi mkubwa wa kwanza wa dhahabu kufikia hatua hii ya maendeleo nchini baada ya karibu miaka 20, na ubia wetu na Serikali ni msingi wa kuhakikisha manufaa yake yanagawiwa kwa haki, yanaonekana na yanadumu kwa muda mrefu," amesema Lupokela.

Katika eneo la mradi lililopo Sengerema mkoani Mwanza, zaidi ya watu 3,600 wanafanya kazi kwa sasa, huku wafanyakazi 281 wakiwa wameajiriwa moja kwa moja na kampuni. Wengi wao ni Watanzania, hususan kutoka katika jamii zinazozunguka mradi huo, hatua inayodhihirisha utekelezaji wa sera ya kutoa kipaumbele kwa nguvu kazi ya ndani.

Ujenzi wa mgodi huo umefikia takribani asilimia 50, huku uwekezaji wa zaidi ya dola za Marekani milioni 250 ukiwa tayari umefanyika. Kwa mujibu wa makadirio ya kampuni, Nyanzaga una hifadhi ya takribani wakia milioni nne za dhahabu na unatarajiwa kuzalisha kwa angalau miaka 16, hali inayotarajiwa kuongeza ajira, mapato ya Serikali na fursa za biashara kwa Watanzania kwa kipindi kirefu.

Mradi huo pia unatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayotambua sekta ya madini kama moja ya nguzo za kukuza uchumi wa viwanda na maendeleo jumuishi.