Sugu: Samia amenifanya nisitishe kuhamishia biashara Malawi, Afrika Kusini

Friday April 16 2021
sugupic

Aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu

By Mwandishi Wetu

Aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu amesitisha mpango wake wa kuhamishia biashara zake mjini Blantyre, Malawi na Afrika Kusini.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram leo Ijumaa Aprili 16, 2021, Sugu amesema amechukua uamuzi huo kuunga mkono hatua zinazochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara Tanzania.

Advertisement