Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafanyabiashara wa tanzanite wakanusha utoroshaji madini

Muktasari:

  • Chama cha wanunuzi na Wauzaji madini Tanzania (TAMIDA) kimekanusha kuwepo kwa utorishaji wa madini na kuiomba Serikali iwadhibiti wanaoeneza habari hizo, kwani zinapoteza soko la madini hayo.

Arusha. Wadau wa madini ya tanzanite wameiomba Serikali kutumia taasisi zake kudhibiti watu wanaoeneza taarifa za upotoshaji kwamba madini hayo yanaendelea kutoroshwa kwa wingi licha kuwepo kwa udhibiti.
Akizungumza juzi Januari 16 na waandishi wa habari mkoani hapa, Mwenyekiti wa Chama cha wanunuzi na Wauzaji  madini Tanzania(TAMIDA), Sammy Mollel amesema athari za kuendelea  kufumbia macho upotoshaji huo ni kubwa na licha ya kuendelea kudumaza soko la madini hayo.
Mollel amesema kuwa wao kama wadau sekta hiyo wamesikitishwa na taarifa hizo na amewataka Watanzania kutoa ushirikiano ukiwemo wa kuwabaini watu wanaoeneza taarifa hizo.
“Tangu kujengwa kwa ukuta katika eneo hilo mwaka 2017 na kufungwa kwa mitambo ya kielektroniki ya ulinzi kumesaidia kuondoa mianya ya utoroshaji wa madini na kwa hali inayoonekana hapa hakuna utoroshaji unaoweza kufanyika kutokana na udhibiti mkubwa uliopo,” amesema Mollel.
Ameongeza  kuwa kama mtu ana uhakika na taarifa hizo ni vizuri akatoa  ushirikiano kwa kutoa ushahidi namna madini hayo yanatoroshwa pamoja na  kuonyesha mianya yote inapopitia ili wanaohusika wachukuliwe hatua.
Naye Ofisa Madini Mkazi Mirerani, Menard Msengi amesema kuwa serikali imeweka ulinzi wa kutosha na mazingira mazuri kuanzia kwenye miradi hadi kufikia sokoni katika kuhakikisha sheria zote zinafuatwa na kwa ulinzi uliopo swala la utoroshaji haliwezi kufanyika hata kidogo.
Kwa upande wake Mwenyekiti  wa Chama cha wanunuzi wadogo wadogo wa madini Tanzania (CHAMATA), Jeremia Kituyo amesema taarifa za kuwepo kwa utoroshaji wa madini zinasababisha  washindwe kufanya biashara, kwani zinawaondolea uaminifu  kwa wateja wao na  wamesisitiza umuhimu vyombo vinavyohusika kufuatilia  na kudhibiti tatizo hilo
"Tunasikitika sana na matamko yanayotolewa yasiyo na ushahidi  kwamba madini yanatoroshwa, ambapo  yanatufedhehesha na kutuvunja moyo  na kuharibu sura  ya biashara ya madini nchini,ambayo matamshi hayo wanaweza kusababisha mataifa mengine kuona kama madini yetu  yana migogoro kitendo ambacho sio kweli," amesema Kituyo.
Mhandisi migodi wa kampuni ya Franone Mining, Benezet Karyuka ameunga mkono hoja hizo, akisema tangu kuwepo kwa ukuta uliojengwa na serikali almaarufu kama ukuta wa Magufuli pamoja na kuondoa  utoroshaji wa madini umewasaidia kuongeza ulinzi ndani ya maeneo  ya uchimbaji.
Baada ya kuwepo kwa uchimbaji holela wa madini hayo ya tanzanite kwa muda mrefu serikali iliamua kufanya maboresho makubwa katika uchimbaji na uuzaji wa madini hayo yakiwemo ya kuweka ukuta na kumarisha mifumo ya uchimbaji ikiwemo kuweka utaratibu  wa kuwatambua wachimbaji wakubwa na wadogo.