Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakulima wapewa mbinu bei ya korosho ipande

Muktasari:

  • Wakulima wazao la korosho wametakiwa kupeleka korosho kwenye maghala ili kuwahi msimu wa mvua.

Liwale. Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Lindi, Cesilia Sositenes  amewataka wakulima wa mazao ya korosho kupeleka kwenye maghala mapema ili kuuza bei nzuri kwa wanunuzi.

 Cesilia ameyasema hayo leo Jumatatu Novemba 6, 2023 kwenye mnada wa korosho wa Chama Kikuu cha Runali, ambapo amesema kuwa msimu unaokuja  wa mvua ili kuepuka kuuza korosho isio na ubora amewataka wakulima kuwahi kupeleka korosho kwenye maghala mapema kwani  ikinyeshewa na mvua inashuka ubora.

"Niwaombe wakulima wa zao la korosho tujitahidi kupeleka kwenye maghala mapema, tunapoelekea ni msimu wa mvua hivyo basi tukichelewa kupeleka korosho zetu mapema zikishaingia unyevu korosho inasababisha kuuzwa kwa bei ya chini," amesema Cesilia.

Baadhi ya wakulima wakifuatilia mnada uliofanyika katika kijiji cha Mkundi Wilayani liwale. Picha na Bahati Mwatesa.

Aidha Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Runali, kinachojumuisha Wilaya tatu, Wilaya ya Ruangwa, Wilaya ya Nachingwea pamoja na Wilaya ya Liwale Odas Mpunga amesema kuwa hadi sasa wakulima wa meshalipwa pesa zao kwa minada miwili,na amewataka wakulima kuacha tabia ya kutumia  account ya mkulima mwingine kwani inaleta changamoto katika malipo.

"Hadi sasa tumeshalipa wakulima wote pesa zao za minada miwili na huu wa tatu hawatachelewa kulipwa fedha zao ila niwaombe wakulima kuacha tabia ya kutumia akaunti ya mkulima mwingine kwani inatupa shida kwenye malipo," Amesema Odas.

Jafari Massoud mkulima wa Kijijj cha Mkundi amewaomba wanunuzi kuongeza bei ili nawao wakulima aweze kunufaika kidogo na zao lao kwani gharama za kulima nikubwa.

"Niwaombe wanunuzi mjitahidi kuongeza bei hata ikiwa 3,000  ili wakulima tuweze kupata faida kidogo baada ya kutolewa makato na Serikali," amesema Jafari.

Faudhia Tella amewaomba wanunuzi kuongeza bei kwa mnada kwani uzalishaji ni mgumu sana, ambapo pia amesema kuwa wakisema hawauzi bei ya korosho itazidi kushuka kutokana na msimu wa mvua unao kuja.

Tunapokwenda ni msimu wa mvua tukisema tukatae kuuza sasa hivi, mvua zikianza korosho inashuka ubora kwa kuwa inakuwa haijakauka, hapo mnunuzi lazima ashushe bei kutokana na kukosa ubora," amesema Faudhia.

 Mhasibu wa Chama Kikuu cha Ushirika  cha Runali, Hashim Abdalla amesema kuwa  zaidi ya tani  8,000 zimeuzwa katika Amcos ya Mkilumani katika Kijiji cha Mkundi kwenye mnada wa tatu huku  bei ya juu ikiwa Sh2,042 na bei ya chini ikiwa Sh1,950.