Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wiki ya utumishi wa umma ilivyogusa maisha ya watu


Muktasari:

  • Katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2026, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) ulitoa vyeti vya kuzaliwa 750 ndani ya siku moja badala ya muda wa kawaida wa siku mbili pia vyeti 10 vya vifo vilitolewa kwa utaratibu wa haraka.

Dodoma. Ndani ya siku nane wananchi wa Dodoma na mikoa ya jirani wamenufaika na huduma mbalimbali kutoka taasisi za umma kwa urahisi ikiwemo kupata vyeti vya kuzaliwa, kupimwa magonjwa mbalimbali na utatuzi wa changamoto zinazowakabili.

Wamepata huduma hizo kupitia maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2026 iliyofanyika kati ya Juni 16 hadi 23, 2026 katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma, yalizikutanisha taasisi za umma kutoka sekta mbalimbali chini ya kaulimbiu isemayo: “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu.”

Akizungumzia ushiriki wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano kwa Umma na Mawasiliano wa Ofisi hiyo, Sabato Kosuri amesema wiki hiyo ni jukwaa muhimu la kuonyesha namna taasisi za umma zinavyowajibika kwa wananchi.

Hilo linafanyika kwa kusogeza huduma karibu na wananchi, sambamba na kutoa fursa ya kupata elimu, ushauri na ufumbuzi wa changamoto katika eneo moja.

Amesema hatua hiyo inaakisi mwelekeo wa Serikali wa kuimarisha utoaji wa huduma kwa kutumia mifumo ya kidijitali na kuongeza uwajibikaji katika sekta ya umma.

“Maadhimisho haya yamethibitisha kuwa taasisi za umma hazisubiri tena wananchi kufika ofisini. Kupitia ushiriki wa OTR na taasisi zinazosimamiwa na Ofisi yetu, wananchi wameweza kupata huduma, elimu na majibu ya changamoto zao kwa wakati, jambo linaloimarisha uhusiano kati ya Serikali na wananchi,” amesema.

Alibainisha kuwa hatua hiyo inaakisi mwelekeo wa Serikali wa kuimarisha utoaji wa huduma kwa kutumia mifumo ya kidijitali na kuongeza uwajibikaji katika sekta ya umma.

“Kupitia ushiriki wa OTR na taasisi zinazosimamiwa na Ofisi yetu, wananchi wameweza kupata huduma, elimu na majibu ya changamoto zao kwa wakati, jambo linaloimarisha uhusiano kati ya Serikali na wananchi,” amesema.

Katika maadhimisho hayo, miongoni mwa taasisi zilizovutia wananchi wengi ni Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) ambao ulitoa vyeti vya kuzaliwa 750 ndani ya siku moja badala ya muda wa kawaida wa siku mbili pia vyeti 10 vya vifo vilitolewa kwa utaratibu wa haraka.

Ofisa Sheria wa Rita, Emmanuela Mwingira amesema zaidi ya wananchi 1,000 walipata elimu kuhusu wosia, usajili wa ndoa na masuala ya bodi za wadhamini.

“Utoaji wa huduma katika maadhimisho hayo umewarahisishia wananchi kupata huduma kwa wakati na kupunguza gharama za usafiri pamoja na muda unaotumika kufuatilia huduma hizo,” amesema.

Katika sekta ya nishati, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) liliwahudumia zaidi ya wananchi 1,500 waliotembelea banda lake. Meneja Masoko wa shirika hilo, Fredrick Kalinga, alisema wananchi walipata elimu kuhusu uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme pamoja na matumizi salama ya nishati hiyo.

Amesema wananchi pia walielimishwa kuhusu mfumo wa Nikonekti unaorahisisha maombi ya huduma za kuunganishiwa umeme kwa njia ya kielektroniki, hivyo kupunguza urasimu, muda wa kusubiri na gharama kwa waombaji.

“Mbali na hilo, pia Tanesco ilitoa elimu kuhusu magari yanayotumia umeme na huduma za wateja zinazopatikana kupitia namba ya bure 180 saa 24 kwa siku,” amesema.

Sekta ya afya nayo ilitumia maadhimisho hayo kutoa huduma za uchunguzi na ushauri bila malipo na miongoni mwake ni Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambapo Afisa Rasilimali Watu wa Hospitali hiyo, Hilda Kajia amesema wananchi 260 walipatiwa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya ngozi, macho pamoja na ushauri wa afya ya uzazi na magonjwa ya wanawake.

“Maonesho hayo yameongeza upatikanaji wa huduma kwa wananchi ambao kwa mazingira ya kawaida huenda wasingeweza kufika hospitalini kwa wakati,” amesema.

Kwa upande wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliwahudumia wananchi 720 kwa vipimo vya shinikizo la damu, sukari, mafuta kwenye damu na uchunguzi wa afya ya moyo.

Meneja wa Huduma za Utawala wa JKCI, Joachim Asenga amesema wananchi waliobainika kuwa na changamoto za kiafya walipewa ushauri, kuanzishiwa matibabu au kupewa rufaa kwa ajili ya huduma zaidi.

Katika upande wa biashara, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (brela) ulitumia maadhimisho hayo kuhamasisha urasimishaji wa biashara.

Ofisa Uhusiano na Mawasiliano Mkuu wa Brela, Theresa Chilambo amesema zaidi ya wananchi 720 walitembelea banda lao huku wateja wapya 400 wakianza mchakato wa usajili kupitia mfumo wa Brela Online System.

Amesema mfumo huo mpya umeongeza uwazi na kupunguza utegemezi wa watu wa kati katika utoaji wa huduma za usajili wa biashara.

Nayo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (Duwasa) iliwahudumia wananchi 157 na kuwaunganishia huduma za maji wateja wapya 26.

Afisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Duwasa, Halima Kambi amesema wananchi walipata elimu kuhusu mfumo wa e-Mrejesho unaowezesha ulipaji wa bili na utoaji wa malalamiko kwa njia ya mtandao bila kufika ofisini.