Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wizi wa mtandao nchini watikisa sekta ya utalii

Muktasari:

 Wageni wanaoingia nchini huombwa kutuma fedha kwenye akaunti feki za kampuni mbalimbali

Moshi. Wizi na utapeli kwa njia ya mtandao, umeanza kuitikisa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha baada ya wahalifu wa kimataifa kuingilia mawasiliano ya baruapepe (emails) za mawakala wa utalii.

Katika kipindi cha miezi miwili, zaidi ya kampuni 10 zimeingiliwa mawasiliano yake na watalii kuelekezwa kutuma fedha kwa watu tofauti kupitia taasisi za fedha ikiwamo Western Union.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa maelfu ya Dola za Marekani yametumwa kwa wezi hao wa kimataifa kupitia taasisi mbalimbali za fedha katika miji ya Kampala nchini Uganda, Moshi na Dar es Salaam (Tanzania).

Katika tukio lililotokea Agosti 25, wezi hao waliingilia mawasiliano ya kampuni moja ya utalii ya wilayani Moshi na kufanikiwa kumwibia mtalii mmoja raia wa Marekani Dola3,500 za Marekani (Sh7.4 milioni).

“Tuliendelea kuwasiliana na mgeni wetu, baadaye alituomba tumjibu maswali fulani kuhusu malipo na baada ya kujibu email (barua pepe) hatukupata tena majibu,” alidai mkurugenzi wa kampuni hiyo.

Mkurugenzi huyo aliyeomba jina la kampuni yake lisitajwe kwa vile jambo hilo liko kwenye uchunguzi, alidai kuwa baadaye aligundua kuwapo kwa mawasiliano asiyoyatambua kwenye akaunti yake.

“Nilishangaa kwenye Inbox (kwenye akaunti) nikashangaa kukuta email mpya ambazo zimeshasomwa zikimwelekeza mgeni atume fedha kwenye akaunti ambayo sio yangu,” alidai mkurugenzi huyo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, walijitahidi kuwasiliana na mtalii huyo lakini hadi wanampata alikuwa  ameshatuma fedha hizo kupitia benki moja nchini.

Polisi wa kitengo cha makosa ya kimtandao, wameanza uchunguzi kujua ilikuwaje benki ikafungua akaunti kwa jina feki na kisha matapeli hao kuweza kuzitoa fedha hizo.

Mkurugenzi wa kampuni ya King of Kilimanjaro Expedition, Shatiel Mhina alidai kuwa siku chache zilizopita, wezi hao waliingilia mtandao wa kampuni yake na kumwibia mgeni wake Dola 6,000 za Marekani (Sh13.2 milioni).

“Nilipofuatilia mawasiliano ya email yangu nikagundua kweli kuna mtu aliingilia mawasiliano na kumwelekeza namna ya kutuma fedha na jina kisha aka delete (akafuta) mawasiliano yale.”

Mkurugenzi wa Topi Adventure Tours&Safaris, Emanuel Kimaro, alidai kuwa mgeni wake aliyetarajiwa kufika nchini mwezi uliopita, aliibiwa pia Dola 1,000 kwa njia kama hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani alisema tatizo liko kwa wanaoibiwa kushindwa kutoa taarifa polisi wanapobaini.

kwa vile kampuni zao hazina leseni ya Tala.

“Mimi kama RPC wa Kilimanjaro sijui ukubwa wa tatizo hilo, lakini nataka nikuambie sio wengi wanafungua kesi, wanaishia kufa na tai shingoni kwa vile kampuni zao haziko kihalali,” alidai kamanda huyo.

Ametoa wito kwa wanaoibiwa kwa njia hiyo kutoa taarifa polisi kwa vile sasa wana kitengo maalum cha kushughulikia makosa hayo na kina wataalamu wa kuweza kubaini wahusika.