Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bobi Wine akamatwa, awekwa 'kizuizini'

Kiongozi wa Upinzani Nchini Uganda, Bobi Wine

Muktasari:

  • Kiongozi wa Upinzani nchini Uganda Bobi Wine alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe jana Alhamisi alipokuwa akirejea nchini, kwa mujibu wa chama chake cha National Unity Platform.

Entebe. Kiongozi wa Upinzani Nchini Uganda, Bobi Wine alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe, jana Alhamisi alipokuwa akirejea nchini, kwa mujibu wa chama chake cha National Unity Platform.

Kupitia video iliyosambaa mitandaoni iliwaonyesha wanaume kadhaa wakimkamata Wine baada tu kushuka kwenye ndege huku mmoja wa washirika wake akipiga kelele mara kadhaa, "Unampeleka wapi?"

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya nyumba yake baada ya kuachiwa, Wine alisema kuwa yuko chini ya kizuizi cha nyumbani.

"Tunapozungumza hivi sasa, niko chini ya kizuizi cha nyumbani kwa sababu nyumba yangu imezingirwa, unajua, askari na polisi wako kila mahali," amesema.

Wine amesema kwamba mara tu alipotua Entebbe, walimkamata na kumweka kwenye “gari la watu ambao walikuwa wakimsubirii” na kwamba lilikuwa nan a watu zaidi ya 15.

"Ilikuwa ya kufedhehesha sana, haikufurahisha, lakini ninafurahi kufika hapa," amesema.

Kukamatwa huko kunaonekana kuwa ni jaribio la kusimamisha maandamano yaliyokuwa yamepangwa na wafuasi wake mara baada ya kutua nchini humo, hata hivyo, polisi tayari ilikuwa imeonya kutoruhusu watu kuandamana.

Boby Wine, mwanasiasa ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, alikuwa mgombea mkuu wa upinzani katika uchaguzi wa urais wa Januari 2021; hata hivyo, Rais Yowel Museveni aliibuka mshindi katika uchagua huo ambao upinzani unaulalamikia.

Wakati katika uchaguzi huo Museveni akijinasibu kuchaguliwa tena katika muhula wa sita licha ya madai mengi ya udanganyifu na vitisho. Hata hivyo Wine alipinga matokeo ya uchaguzi huo, akisema alikuwa na ushahidi wa udanganyifu na vitisho.

Wine aliporejea nchini humo, Jukwaa la Umoja wa Kitaifa pia lilidai kuwa makao yake makuu yamezingirwa na maofisa wa polisi.

Chama chake pia kilisema kwenye mtandao wa X helikopta za kijeshi zimerekodiwa zikipita juu ya paa la nyumba ya Wine huko Magere, Uganda, na kuongeza kuwa maofisa wa usalama wametumwa kuzunguka uzio wa nyumba yake.

Kwa miaka kadhaa sasa, Wine amekuwa akikabiliwa na hali ya kukamatwa kamatwa na vikosi vya usalama vya Uganda, na hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi uliokumbwa na utata nchini humo.

Siku ya Alhamisi akiwa anajiandaa kurejea nchini humo, Wine aliandika kwenye ukurasa wake wa X (zamani Twitter) akisema, “Hata nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya kwa kuwa Bwana yu pamoja nami - Zaburi 23:4. Narudi nyumbani!”

Jeshi la Polisi la Uganda lilitoa taarifa Jumatano likisema wamepokea taarifa kuhusu maandamano yaliyopangwa kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe siku ya Alhamisi, yakihusisha "kundi la wanaharakati wa kisiasa, wanaohusishwa na Jukwaa la Umoja wa Kitaifa (NUP)."

Polisi waliwahimiza waandaaji kufuta maandamano hayo ili kuepusha usumbufu wa magari na hatari ya kuvutia vitendo vya kihalifu dhidi ya madereva wa magari, abiria, na wafanyabiashara kupitia vitendo vya wizi au vitendo vingine vya uhalifu.

"Pia tunushauri umma ambao unaweza kuwa umehamasishwa, ujizuie kushiriki katika shughuli hizi haramu," taarifa ya polisi iliyotolewa Jumatano ilisema.

"Vyombo vya usalama vitachukua hatua zote zinazohitajika ili kuhakikisha kuwa watu wanaohusika katika shughuli hiyo haramu wanakamatwa na kufikishwa mbele ya mahakama,” iliongeza taarifa hiyo.

Imeandikwa na Victor Tullo kwa msaada wa mashirika