Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Canada yamchagua Spika wa kwanza mweusi

Muktasari:

  • Mbunge kutoka Chama cha Liberal nchini Canada, Greg Fergus amechakuliwa kuwa Spika mpya, akichukua nafasi ya Anthony Rota ambaye alijiuzulu wiki iliyopita, kufuatia shutuma baada ya kumwalika mfuasi wa zamani wa Adolf Hitler.

Dar es Salaam. Mbunge kutoka Chama cha Liberal nchini Canada, Greg Fergus amechaguliwa kuwa Spika mpya, akichukua nafasi ya Anthony Rota ambaye alijiuzulu wiki iliyopita, kufuatia shutuma baada ya kumwalika mfuasi wa zamani wa Adolf Hitler.

Hitler alikuwa dikteta wa wa Ujerumani kuanzia mwaka 1933 hadi kifo chake 1945, na kwamba Rota alimualika mkongwe wa zamani wa Vita vya Pili vya Dunia ambaye alipigana pamoja na Wanazi (waliomuunga mkono Hitler), kuhudhuria Bunge wakati wa hotuba ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy bungeni hapo.

Hata hivyo, Rota alijitetea kwa kusema kuwa alikuwa hafahamu uhusiano wa Wanazi wa Varoslav Hunka, 'akin' maisha yake ya nyuma yalipojulikana, kosa hilo lilishika vichwa vya habari vya kimataifa na ilikuwa aibu kubwa kwa Canada.

Kwa mujibu wa mtandao wa TRT Afrika, tukio hili la Jumanne Oktoba 3, 2023; la kumchagua mcanada mweusi kuwa kiongozi wa chombo hicho maarufu kama 'House of Commons', linaashiria ukurasa mpya katika historia ya nchi hiyo.

Fergus alikuwa miongoni mwa wabunge saba wanaotaka kujaza nafasi ya spika Rota ambayo kimsingi ni kudhibiti mienendo ya wabunge na kuongoza ajenda na kusuluhisha mijadala.

Mara kwa mara, Wabunge katika chombo hicho, hugeuza baraza hilo na kuwa jukwaa la kurushiana maneno makali, kuzozana na kudhalilishana. Hivyo Spika mpya amesema anatumaini kuchaguliwa kwake kutarejesha utulivu na heshima ya chombo hicho.

"Heshima na adabu - nitafanya kazi kwa bidii katika hili na ninahitaji usaidizi wenu nyote kufanikisha hili," Fergus amesema hayo akiwa katika kiti cha spika, alipokuwa akitoa hotuba yake kwa wabunge baada ya kuchaguliwa kwa kura ya siri.

"Heshima ni sehemu ya msingi ya kile tunachofanya hapa," amesema. "Tunahitaji kuhakikisha kwamba tunaheshimiana na tunawaonyesha raia wetu mfano huo. Hatuwezi kuwa na mazungumzo isipokuwa kuwe na maelewano ya kuheshimiana."

Waziri Mkuu Justin Trudeau amesema anatumai Fergus amefanikiwa katika azma yake.

"Tulikuchagua ili utusaidie kuwa wastaarabu katika mijadala yetu, ili kutukumbusha sisi sote tuko hapa kwa sababu moja, ambayo ni kuwatumikia Wacanada," Trudeau amesema.

Mambo kadhaa kumhusu Spika mpya

Fergus ambaye ni Mbunge wa Chama cha Liberal cha Waziri Mkuu wa nchi hiyo, amekuwa akijitambulisha kama ni mwanaharakati wa jamii, mtu mwenye mawazo chanya, mkimbiaji wa mbio ndefu, babu na mwanamuziki ‘aliyefeli.’

Ana shahada mbili za awali katika sayansi ya kijamii na katika uhusiano wa kimataifa, pia ana shahada ya uzamili katika uhusiano wa kimataifa.

Amewahi kufanya kazi katika katika sekta binafsi na umma, na mashirika yasiyo ya faida na katika sekta ya kitaaluma. Pia ameshika nyazifa mbalimbali ndani ya chama chake cha siasa ikiwa ni pamoja na kuwa mkurugenzi chama kitaifa.

Fergus alichaguliwa kwa mara ya kwanza kama mbunge mwaka 2015, lakini pia katika chaguzi za 2019 na 2021.

Amehudumu kama Katibu wa Bunge wa Waziri Mkuu, Rais wa Bodi ya Hazina, Waziri wa Serikali ya Kidijitali na Waziri wa Viwanda. Pia alikuwa mjumbe wa kamati kadhaa za Baraza la ‘Commons,’ ikiwa ni pamoja na fedha. Aliongoza kikao cha wabunge Weusi

Fergus ameoa, na ana watoto watatu na wajukuu wawili.