DRC yamfukuza balozi wa Rwanda, yampa saa 48

Vincent Karega

Muktasari:

  • M23 ni kundi la waasi ambalo mamlaka ya Kongo inashutumu Rwanda kwa kuunga mkono lakini Rwanda inakanusha, liliteka mji wa Kiwanja mashariki mwa Kongo siku ya Jumamosi, na kuukata mji mkuu wa Kivu Kaskazini Goma kutoka nusu ya juu ya jimbo hilo.

Dar es Salaam. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imemfukuza balozi wa Rwanda nchini humo, Vincent Karega huku ikimpa saa 48 kuondoka nchini humo.

 Hatua hiyo inakuja wakati kundi la waasi la M23 ambalo Congo inadai linaungwa mkono na Kigali, likiendelea kupata nguvu huko mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa ya Msemaji wa Serikali ya Congo, Patrick Muyaya imesema kutokana na Rwanda kuendelea kuunga mkono M23, baraza la ulinzi linaloongozwa na Rais Felix Tshisekedi limeamua kumpa balozi huyo saa 48 kuondoka nchini humo.

"Hii ni kwa kiasi fulani, kutokana na kuendelea kwa nchi ya (Karenga) kushambulia DRC na kuunga mkono harakati za kigaidi za M23," imesema taarifa hiyo

Uamuzi wa kumtimua balozi wa Rwanda umefikiwa baada ya Serikali ya Congo kufanya tathmini juu ya hali ya usalama nchini humo.

M23 ni kundi la waasi ambalo mamlaka ya Kongo inashutumu Rwanda kwa kuunga mkono lakini Rwanda inakanusha, liliteka mji wa Kiwanja mashariki mwa Kongo siku ya Jumamosi, na kuukata mji mkuu wa Kivu Kaskazini Goma kutoka nusu ya juu ya jimbo hilo.