Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Familia ya kijana anayedaiwa kufia gerezani kwa kunguni yataka uchunguzi

Muktasari:

  • Familia ya LaShawn Thompson aliyepoteza maisha akiwa gerezani baada ya kung’atwa na kunguni yataka uchunguzi wa kifo cha ndugu yao ufanyike.

Dar es Salaam. Familia moja kutoka Jimbo la Georgia nchini Marekani inataka uchunguzi ufanyike kutokana na kifo cha ndugu yao aliyefariki akiwa katika gereza la Fulton alipokuwa anatumikia kifungo baada ya kudaiwa kung'atwa na kunguni.

 Kwa mujibu wa vitu vya habari nchini humo vimeeleza kuwa LaShawn Thompson, mwenye umri wa miaka 35, alipatikana akiwa amefariki gerezani baada ya kung’atwa na kunguni Septemba 2022.

Wakili wa familia hiyo alitoa picha zinazoonyesha mwili wa Thompson ukiwa umejaa kunguni huku akieleza kwamba gereza alilokuwepo Thompson kipindi cha uhai wake, haikufaa hata mnyama kuishi.

Hata hivyo, kulingana na ripoti ya Mkaguzi wa Matibabu inaeleza kwamba Thompson alipatikana akiwa hana fahamu akiwa gerezani miezi mitatu baada ya kukamatwa.

Ripoti ya mchunguzi wa afya wa Kaunti ya Fulton ilibainisha bado sababu za kifo cha Thompson bado hazijajulikana na alibainisha kulikuwa na uvamizi mkali wa kunguni kwenye seli yake.

Kulingana na mtaalamu wa wadudu katika Chuo Kikuu cha Kentucky, ambaye ni mtaalamu wa kunguni, ameeleza kuumwa na kunguni kwa kawaida hakusababishi kifo.

Hata hivyo, katika baadhi ya matukio nadra, Potter alisema, kuwa katika mazingira ya mrundiko wa kunguni kwa muda mrefu kunaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini yaani anemia kali, ambayo inaweza kuwa mbaya ikiwa haitatibiwa.


Imeandaliwa na Emmanuel Msabaha.