Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gachagua amtaka bosi wa Usalama ajiuzulu

Muktasari:

  • Rigathi Gachagua amemshushia zigo la maandamano bosi wa Usalama, amtaka ajiuzulu

Nairobi. Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua amemtaka Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa hilo, Noordin Haji ajiuzulu kutokana na kushindwa kumshauri Rais William Ruto vizuri kuhusu sakata la maandamano ya Gen Z.

Gachagua amesema kama bosi huyo wa Usalama angemfahamisha vyema Rais Ruto kuhusu ukubwa wa maandamano hayo, maandamano yasingetokea na wala yasingefika huko.

"Habari hizi hazikupatikana kwa Rais Ruto, angejua kuwa wananchi hawakuutaka Mswada wa Fedha wa 2024 angewataka watu wake waifute. Hata hivyo, tuna shirika (NIS) ambalo limelipwa kutoa taarifa kama hizo. Ni wazi kuna kushindwa katika ujasusi," amesema.

Pia, amesikitika kuwa kutokana na kutofanya kazi vizuri kwa NIS, maisha ya watu yamepotea na mali ya mamilioni ya fedha zimeharibiwa.

"Maofisa wakuu wameniambia kwa faragha kwamba hawakuwa na taarifa ya kijasusi kuhusu maandamano," amesema.

Wakati huo, Gachagua ametoa wito wa kufanyika mazungumzo, ili kuepuka kujirudia kwa maandamano ya kupinga muswada wa fedha yaliyotikisa nchini humo tangu Jumanne ya Juni 18, 2024.