Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kijana wa miaka 17 aiba ndege ya jirani yake, apaa nayo na kugonga miti

David Chege, akiwa chini ya ulinzi

Muktasari:

  • Kijana huyo aliangalia kwa jirani na kuona kuna ndege iliyokuwa imeegeshwa na akaamua kwenda kuingia akaiwasha kisha akapaa nayo kwa bahati mbaya  akagonga miti, taarifa zinasema amekamatwa na maafisa wa polisi na anasaidia katika kuchunguza tukio hilo la Ijumaa.

Kenya. David Chege kijana mdogo mwenye umri wa miaka 17, amewaacha watu vinywa wazi baada ya kuiba ndege ya jirani yake iliyokuwa imepaki na kuirusha bila woga, tovuti ya TUKO imeripoti.

Siku ya Ijumaa Machi 24, Chege anadaiwa kuingia kwa siri kwenye nyumba ya jirani yao ambaye ni mzungu na kufaulu kufika eneo la rubani na kufanikiwa kuiwasha kisha kuruka nayo kwa dakika kadhaa kabla ya kuparamia miti.
 
Mwenye ndege hiyo yenye usajili wa nambari 5Y-AZA aina ya PA25 aliwambia polisi kuwa kijana aliingia kwake asubuhi kinyemera na kutekeleza uharifu huo.

Iliripotiwa kuwa mwenye ndege hiyo ambaye ni mkaazi wa Balolow eneo la Ndume Gilgil alisema "saa 9:30 asubuhi kuna mtu aliingia kwake na kuipaisha ndege iliyokuwa imeegeshwa," taarifa ya polisi ilisema.
 
Katika taarifa nyingine mbunge wa Kapseret, Oscar Sudi ameahidi kuhakiksiha kuwa atamsimamia Chege kusoma urubani.
 
"Naomba serikali kumsamehe huyu kijana kutoka Gilgil asishtakiwe, tafadhali mnipatie ili nimpeleke katika chuo cha kujifunza mambo ya kuwa rubani," alisema Sudi.