Kim Jong-un, Donald Trump wakutana Korea

Donald Trump amekutana na kufanya mazungumzoa na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un katika eneo la kati ya nchi hiyo na Korea Kusini.

Baada ya kukupiga picha wakishikana mkono, Trump na Kim wamefanya mazungumzo karibu kwa saa moja, ambapo walikubaliana kufufua mazungumzo  yaliyokwama kuhusu masuala ya nyuklia.

Mkutano wao wa mwisho ulivunjika Februari bila makubaliano yoyote kuhusu kusitisha mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Viongozi hao wamekutana katika eneo lisilokuwa  na  shughuli  za  kijeshi linalozigawa nchi hizo, tangu kumalizika kwa uhasama na kivita mwaka 1953.

Mkutano huo uliandaliwa na Trump kwa kumwalika Kim kupitia Twitter.

“Ni vizuri nimekuona tena. Sikutarajia kukutana na wewe mahali hapa,” Kim amemweleza Trump kupitia mkalimani mbele ya vyombo vya habari vilivyorusha tukio hilo moja kwa moja.

“Ni wakati mziri sana...Ni mafanikio makubwa,” amesema Trump.