Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maelfu wajitokeza kuuaga  mwili wa Khamenei Tehran

Muktasari:

  • Kifo cha Khamenei kilitokea Februari 28, 2026, kufuatia shambulio la anga lililoripotiwa kufanywa kwa pamoja na Marekani na Israel

Dar es Salaam. Shughuli rasmi za kuagwa mwili wa aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khame-nei, zimeanza leo mjini Tehran, zikivuta maelfu ya waombolezaji katika tukio kubwa la kitaifa linaloendeshwa chini ya ulinzi mkali na hali ya taha-ruki ya kisiasa Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa taarifa za Serikali ya Iran, maombolezo hayo yataendelea kwa siku sita yakihusisha mzunguko wa kuaga mwili katika miji kadhaa muhimu ya kidini kabla ya mazishi ya mwisho yanayotarajiwa kufanyika Julai 9, 2026 katika Mji wa Mashhad, alikozaliwa Khamenei.

Mwili wake umeanza kuagwa rasmi Tehran kuanzia Julai 4, 2026 ambako jeneza limewekwa katika eneo maalumu la kitaifa kuruhusu wananchi, viongozi wa serikali, wanajeshi na viongozi wa kidini kutoa heshima za mwisho.

Baada ya hatua hiyo, ratiba inaonesha mwili huo utapelekwa katika mji mtakatifu wa Qom kwa ibada za kidini, kisha kuelekea Iraq kwa heshima za kiroho kabla ya kurejea Iran kwa maziko ya mwisho.

Kifo cha Khamenei kilitokea Februari 28, 2026, kufuatia shambulio la anga lililoripotiwa kufanywa kwa pamoja na Marekani na Israel.

Tukio hilo lilitikisa siasa za kikanda na kuibua hofu ya kuongezeka kwa mgogoro mpana wa kijeshi kati ya mataifa makubwa na Iran.

Katika mitaa ya Tehran, hali ya maombolezo imechanganyika na hisia kali za kisiasa. Maelfu ya waombolezaji wameonekana wakibeba mabango mekundu na alama mbalimbali za kisiasa, ishara inayoonesha sio tu huzuni bali pia hasira na wito wa kulipiza kisasi.

 Vikosi vya usalama vimeimarishwa, vikidhibiti mikusanyiko mikubwa huku baadhi ya barabara zikifungwa kwa muda ili kuruhusu shughuli hizo kufanyika kwa utulivu.

Mamlaka za Iran zimesisitiza kuwa shughuli hiyo ni ya kitaifa na inapaswa kufanyika kwa heshima na utulivu, licha ya hisia kali zinazoendelea kuon-ekana miongoni mwa wananchi ku-husiana na mvutano katika ukanda huo.

Tukio hilo linafanyika huku mwanga wa mazungumzo ukianza kurejesha matumiani kwa pande zote ambapo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema ma-zungumzo ya awali yameanza kuweka msingi wa makubaliano mapya ya-nayolenga mpango wa nyuklia wa Iran pamoja na masuala ya usalama wa kikanda.

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif amesema kuna dalili za uwezekano wa kufikiwa makubaliano ya haraka ya amani, akieleza kuwa mazingira ya sasa yan-aweza kufungua ukurasa mpya wa di-plomasia katika eneo hilo lenye migo-goro ya muda mrefu.

Hata hivyo, Rais wa Marekani, Don-ald Trump, amesisitiza kuwa maku-baliano yoyote lazima yajumuishe udhibiti mkali wa mpango wa nyuklia wa Iran na mfumo wa ufuatiliaji wa kimataifa, akionya kuwa usalama wa kikanda hauwezi kuachwa bila udhibiti wa wazi.

Aidha, dunia inafuatilia kwa karibu hatua za mazishi hayo, huku macho yote yakielekezwa Mashhad ambako Khamenei anatarajiwa kuzikwa rasmi Julai 9, 2026 hatua itakayohitimisha tukio hilo ambalo ni moja ya maom-bolezo makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Iran katika miaka ya hivi karibuni.