Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maporomoko ya ardhi yaua 21 Indonesia

Muktasari:

  • Eneo lililoathiriwa ni kisiwa cha Sumatra ambapo mbali na watu 21 kufariki, pia watu sita hawajulikani walipo mpaka sasa.

Indonesia. Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mafuriko nchini Indonesia imefikia 21.

Taarifa kutoka nchini humo zinasema eneo lililoathiriwa ni katika kisiwa cha Sumatra ambapo watu sita hawajulikani walipo mpaka sasa.

Mvua kubwa iliyonyesha Alhamisi, Macho 7, 2024  ilisababisha maafa katika eneo la Pesisir Selatan katika jimbo la Sumatra Magharibi, huku zaidi ya watu 75,000 wakilazimika kuhama.

"Hadi kufikia leo Jumapili, watu 21 wamepatikana wakiwa wamekufa na watu sita wametoweka," Fajar Sukma, ofisa kutoka shirika la kukabiliana na majanga la Sumatra Magharibi, ameiambia AFP.

Sukma amesema kijiji kilichoko kando ya mlima katika kitongoji cha Sutera kimekumbwa na maafa hayo, huku takriban familia 200 zikiachwa bila makazi.

Naye, Doni Gusrizal, ofisa mkuu kutoka shirika la kukabiliana na maafa la Pesisir Selatan, amesema maji yameanza kupungua baada ya mafuriko, lakini bado ni vigumu kuyafikia maeneo yaliyoathiriwa.

Mara kadhaa Indonesia hukabiliwa na maporomoko ya ardhi wakati wa msimu wa mvua na tatizo hilo limekithiri katika baadhi ya maeneo kutokana na ukataji miti, huku mvua inayonyesha kwa muda mrefu ikisababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo ya taifa hilo la visiwa.

Maporomoko ya ardhi na mafuriko yalisomba makumi ya nyumba na kuharibu hoteli karibu na Ziwa Toba huko Sumatra Desemba mwaka jana na kuua watu wasiopungua wawili.


Imeandaliwa na Sute Kamwelwe na Mashirika