Odinga aendelea kulia na matokeo ya urais Kenya

Muktasari:

  • Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ameendelea kusisisitiza kuwa yeye ndiye mshindi halali wa uchaguzi wa mwaka jana na kuzidisha madai ya udanganyifu miezi mitano baada ya uchaguzi.

Kenya. Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesisitiza kuwa yeye ndiye mshindi halali wa uchaguzi uliofanyika mwaka jana.

Shirika la habari la (VOA) Swahili limeripoti kuwa Odinga alienda mbali zadi na kusema kulikuwa na madai ya udangayifu miezi mitano mara tu baada ya uchaguzi.

Odinga mwenye umri wa miaka 78, alishindwa kwa idadi ndogo ya kura na William Ruto, kulingana na matokeo rasmi, licha ya kuungwa mkono na chama kilichokuwa madarakani.


“Tuna uhakika bila shaka, kwamba ushindi wetu uliibiwa,” mkongwe huyo wa kisiasa jana Jumatatu, aliuambia mkutano uliohudhuriwa na maelfu ya watu mashariki mwa mji mkuu Nairobi.

Akitaja takwimu kutoka kwa mtoa taarifa za siri ndani ya tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) iliyosimamia uchaguzi huo, Odinga alidai alishinda kwa zaidi ya kura milioni mbili.

Baada ya matokeo kutangazwa, alidai kulikuwa na udanganyifu na udukuzi wa seva za tume ya uchaguzi na kupinga matokeo katika kesi ambayo haikufaulu iliyowasilishwa kwenye mahakama ya juu ya Kenya.