Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pinda agusia utapiamlo, wadau wataja kuadimika kwa mbogamboga

Muktasari:

  • Akizungumzia hali ya uelewa wa vyakula vya mbogamboga katika jamii, Dk Sognigbe N’Danikou ambaye ni mwanasayansi na mtafiti kutoka Taasisi ya World Vegetable Center amesema: “Uelewa juu ya aina mbali mbali za mbogamboga za kiasili zimepotea kwa jamii nyingi za kiasili za Kiafrika.

Rwanda. Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Mizengo Pinda amesema ili kumaliza tatizo la utapiamlo ni lazima ulaji wa chakula bora chenye mbogamboga uhimizwe nchini.

Pinda ameyasema hayo katika uzinduzi wa mkakati kabambe wa miaka 10 wa mambo ya chakula barani Afrika uliofanyika Kigali nchini Rwanda Septemba 2-6, 2024.

Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya World Vegetable Center kwa kushirikiana na Crop Trust, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika pamoja na Tume ya Umoja wa Afrika umezindua mkakati kabambe wa kunusuru vinasaba vya mbogamboga za asili ya Kiafrika ambazo uwepo wake unatishiwa kutoweka.

Akizungumzia hali ya uelewa wa vyakula vya mbogamboga katika jamii, Dk Sognigbe N’Danikou ambaye ni mwanasayansi na mtafiti kutoka Taasisi ya World Vegetable Center amesema: “Uelewa juu ya aina mbali mbali za mbogamboga za kiasili zimepotea kwa jamii nyingi za kiasili za Kiafrika.

“Afrika ni nyumbani kwa aina nyingi za mboga mboga ambazo uwepo wake unatishiwa kutoweka haswa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na ukuaji wa miji. Kwa mfano aina ya cowpeas ambayo ni ya mwituni ikiwa na asili ya Afrika tayari imeshatoweka,” alisema Dk N’Danikou.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mkuu wa World Vegetable Center kwa ukanda wa Afrika Dk Gabriel Rugalema alisema mabadiliko ya tabia nchi na ukuaji wa miji ni baadhi ya sababu zinazopelekea kutoweka kwa baadhi ya mboga mboga za kiasili za Kiafrika.

“Athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, ukame, mafuriko, ukuaji wa miji ni baadhi ya sababu zinazohatarisha uwepo wa mbogamboga za kiasili za Kiafrika. Mkakati huu wa miaka 10 unalenga kuwaleta pamoja wadau mbali mbali kwa ajili ya kuokoa mboga mboga za kiasili za Kiafrika,” alieleza.

Pia, Dk Rugalema aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo, kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 12 kitahitajika kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo. Mpango utagusa maeneo manne ikiwa ni pamoja na kuokoa, uhifadhi, kuandaa na kusambaza mbegu pamoja na taarifa, ushirikiano, kutengeneza sera wezeshi pamoja na elimu.

Dk Sognigbe alisema ili kuzuia hali hiyo kuna haja ya kuwekeza kwenye miundo mbinu katika ngazi ya nchi ili kuwepo na benki ya mbegu ambazo zitasaidia kuendeleza upatikanaji wa mbegu na kuondoa uwezekano wa kutoweka kwa mbegu za asili.

“Mpango huo pamoja na mambo mengine utakusanya mbegu za aina mbali mbali kiwa ni pamoja na hizi za mwituni lengo likiwa ni kuzihifadhi na kuzizalisha. Zaidi ya asilimia 90 ya mbegu zinazotumika barani Afrika zinatoka kwa wakulima ambao huhiziifadhi kila wanapovuna. Kama utaratibiu huu utatekelezwa kikamilifu, utasaidia utaratibu wa kuhifadhi mbegu za asili za kiafrika,”ameongeza Dk Sognigbe.