Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Jinping ahimiza ushirikiano China, Afrika

Muktasari:

  • Serikali ya China imekuwa mshirika mkubwa na mataifa ya Afrika ambapo, yamekuwa yakishirikiana kwenye biashara, utamaduni na teknolojia.

Beijing, China. Rais wa China, Xi Jinping ametuma ujumbe wa pongezi kwa viongozi ya mataifa ya Afrika wakati wa mkutano wa 36 wa Umoja wa Afrika (AU), huku akisisitiza kwamba, nchi yake itaendelea kushirikiana na nchi hizo.

Katika ujumbe wake huo, Rais Xi amedokeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, AU imeungana na kuziongoza nchi za Afrika kutatua changamoto za kimataifa, kuharakisha ujenzi wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) na kuwa kwenye nafasi muhimu ya upatanishi wa masuala ya mizozo.

Ameongeza kuwa hadhi ya kimataifa na ushawishi wa mataifa ya Afrika duniani umeendelea kuongezeka.

"Ninazitakia kwa dhati nchi za Afrika na watu wake mafanikio makubwa katika kuelekea kwenye maendeleo na ufufuaji," amesema Xi.

Amesisitiza kuwa uhusiano kati ya China na Afrika umedumisha kasi nzuri ya maendeleo mwaka 2022 kwani, ushirikiano kati ya China na Afrika umeendelea kustawi kwa pande zote, ngazi mbalimbali na ubora wa hali ya juu, na iko mstari wa mbele katika ushirikiano wa kimataifa na Afrika.

Xi amesema yuko tayari kufanya kazi na viongozi wa Afrika ili kuimarisha zaidi urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika, kuratibu na kushirikiana kwa karibu katika masuala ya kimataifa na kikanda, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya ngazi ya juu ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.