Senegal wapiga kura leo baada ya vurugu

Wapiga kura wakiwa kwenye foleni wakisubiri kituo cha kupigia kura kifunguliwe huko Dakar, Senegal leo Machi 24, 2024 wakati wa uchaguzi wa rais wa Senegal. Raia hao watapiga kumchagua rais mpya katika kinyang'anyiro kisichotabirika baada ya miaka mitatu ya machafuko na mzozo wa kisiasa.  Picha na AFP

Muktasari:

  • Raia wa Senegal leo wanapiga kura kumchagua Rais mpya baada ya wiki kadhaa za vurugu za kisiasa. Wagombea 17 wanashiriki katika uchaguzi huo, ambao unatajwa kuwa mgumu.

Dakar, Senegal/AFP. Baada ya wiki kadhaa za vurugu za kisiasa, Raia wa Senegal leo Jumapili Machi 24, 2024 wanapiga kura ya kumchagua Rais atakayeongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Kinyang’anyiro hicho kinawahusisha wagombea 17, huku Rais aliyepo madarakani, Macky Sally akibaki kando baada ya kufikisha kikomo cha awamu mbili za utawala.

BBC inasema uchaguzi huo awali ulipaswa ufanyike Februari 25 lakini Rais Sally aliuahirisha hadi Machi 24 na kusababisha maandamano ya vyama vya upinzani na mzozo wa kidemokrasia.

Katika uchaguzi huo unaotajwa kuwa mgumu, watu milioni 7.3 wanatarajia kupiga kura.

Miongoni mwa wanaowania nafasi hiyo ni pamoja na mgombea wa muungano wa BBY, Waziri Mkuu wa zamani, Amadou Ba (62) na mpinzani wake mkubwa akiwa Bassirou Diomaye Faye (44), ambaye aliachiliwa kutoka jela wiki iliyopita, baada ya kushikiliwa tangu Aprili 2023 kwa mashtaka ya uasi, ambayo alidai yalichochewa kisiasa.

Wote wawili walikuwa wakaguzi wa kodi lakini sasa wanaonekana kuwa na uhusiano mdogo. Ba, mwenye anatoa ahadi za mwendelezo huku Faye akiahidi mabadiliko makubwa.

Wote wawili wanasema watapata ushindi kwenye raundi ya kwanza -- lakini duru ya pili inaonekana kuwa na uwezekano kutokana na kuwepo wagombea wengine 15 katika kinyang’anyiro hicho, akiwemo mwanamke mmoja.

Meya wa zamani wa Dakar, Khalifa Sall (68) anachukuliwa kuwa hana nafasi ya kushinda.

Mshindi atakayeibuka atakuwa na jukumu la kuiongoza Senegal iliyotulia kutoka katika matatizo yake ya hivi majuzi na kusimamia mapato kutokana na akiba ya mafuta na gesi, ambayo yanakaribia kuanza uzalishaji.

Upigaji kura utamalizika jioni na matokeo rasmi ya kwanza yanatarajiwa katika wiki ijayo.

Senegal kwa jadi imekuwa ikizingatiwa kuwa kinara wa demokrasia na utulivu katika eneo lililokumbwa na mapinduzi, ambapo Russia inaimarisha ushawishi wake.

Mamia ya waangalizi watakuwepo wakiwakilisha mashirika ya kiraia, Umoja wa Afrika, kundi la kikanda la ECOWAS na Umoja wa Ulaya.

Kampeni mbaya zilizochukua wiki mbili pekee baada ya kufupishwa, zilifuatia kucheleweshwa kwa dakika za mwisho kwa tarehe ya uchaguzi kutoka Februari 25.

Hatua ya Rais Macky Sall kuingilia kati kuchelewesha uchaguzi wa urais ilisababisha machafuko yaliyosababisha vifo vya watu wanne.

Sall, ambaye alijizolea sifa kimataifa baada ya kukataa ushawishi wa kuwania muhula wa tatu, alisema amesitisha uchaguzi huo kwa hofu kwamba hangekwenda sawa.

Baada ya majuma kadhaa ya mzozo wa kisiasa, Baraza Kuu la Kikatiba la nchi hiyo liliingilia kati na kumlazimisha kuweka tarehe upya Machi 24, licha ya kugongana na mfungo wa Ramadhani.

Mrithi aliyechaguliwa kwa mkono na Rais, Sall Amadou Ba amejinadi kuwa raia wamchague mwenye uwezo na mzoefu badala ya watu watakahitaji miaka miwili kujifunza.

"Hatuhitaji maafisa wanaohitaji miaka miwili ya mafunzo," Ba alisema katika mkutano wake wa mwisho wa kampeni siku ya Ijumaa.

"Tunahitaji kujumuisha tulichonacho. Tunahitaji kwenda kwa kasi zaidi na zaidi."

Ameapa kuunda nafasi za ajira milioni moja katika miaka mitano -- lakini pia atakabiliwa na upande mbaya wa urithi wa Sall, ambao ni pamoja na kukamatwa kwa watu wengi, ukosefu wa ajira na umaskini unaoendelea.


Marekebisho makubwa

Machafuko ya hivi majuzi yalikuwa sura ya hivi punde zaidi katika matukio ya ghasia tangu 2021, yaliyochochewa na mzozo kati ya kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko na Serikali.

Mivutano ya kiuchumi na kijamii, pamoja na wasiwasi kwamba Sall angewania muhula wa tatu, pia vilichochea machafuko yaliyosababisha makumi ya watu kuuawa na mamia kukamatwa.

Uchaguzi huo pia umechochewa na sheria ya msamaha iliyopitishwa kwa haraka iliyopelekea viongozi wa upinzani Faye na Sonko kuachiliwa huru Machi 14 kutoka jela.

Ingawa Faye ni naibu wa Sonko, yuko pekee kwenye karatasi za kura kwa sababu Sonko amezuiwa kusimama machoni pa wapiga kura.

Wawili hao wamemshambulia Ba kama "hatari kubwa zaidi inayokabili Senegal leo".

Pia wamehoji utajiri wake umetoka wapi, wakimtaja kuwa "bilionea mtumishi wa Serikali" ambaye "atakuwa rais wa nchi za kigeni".

Faye aliahidi Ijumaa kuleta "mageuzi makubwa" kwa Senegal, ili kujadili upya mikataba ya madini, mafuta na gesi na ulinzi, wakati huo huo akitoa hakikisho kwa wawekezaji wa kigeni.

"Kuanzia sasa tutakuwa nchi huru, huru, ambayo itafanya kazi na kila mtu, lakini kwa ushirikiano wa kushinda na kushinda," alisema.