Shambulio la anga DRC laua 18, majeruhi 12

Muktasari:
- Watu wenye silaha walishambulia kijiji kimoja katika mkoa wa Ituri, mashariki mwa Kongo jana Alhamisi, na kuua takribani watu 18 na kujeruhi 12.
Kongo. Watu wenye silaha walishambulia kijiji kimoja katika mkoa wa Ituri, mashariki mwa Kongo jana Alhamisi, na kuua takriban watu 18 na kujeruhi 12, afisa wa eneo hilo amesema.
Eneo hilo limekuwa likikabiliwa na maelfu ya makundi yenye silaha huku ghasia zikiwalazimu mamilioni kukimbia makazi yao.
Kanali Jean Siro Simba Bunga, msimamizi wa eneo la Irumu ambapo shambulio limetokea, amesema japo washambuliaji wamechoma na kuteketeza miili mitatu, miili mingine 15 itazikwa.
"Tunasikitishwa na kitendo hiki, tunalaani wanamgambo hao kwa kufanya shambulio hilo katika eneo letu na kusasabisha vifo visivyo vya lazima," amesema Bunga
Alain Kalito aliyenusurika katika shambulio hilo, amesema watoto ni miongoni mwa waathirika wakubwa na kwamba baba yake amejeruhiwa vibaya.
Christopher Munyanderu, mratibu wa shirika la haki za binadamu la Kongo katika eneo la Irumu, amesema shambulio hilo limesababisha watu wengi kukimbia makazi yao
"Shambulio hili linalaaniwa na kila mtu kwa sababu lilikuwa ni shirika ambalo idadi ya watu walikua wakianza kupona taratibu, lakini sasa watu wengi wamehama makazi yao," alisema Munyanderu.