Waangalizi watilia shaka Uchaguzi Zimbabwe

Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa anayewania urais kwa muhula wa pili nchini humo akipiga kura katika uchaguzi uliofanyika Jumatano wiki hii.
Muktasari:
Waangalizi wa uchaguzi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika wamekosoa mwenendo wa uchaguzi nchini Zimbabwe ambapo kura zinahesabiwa.
Zimbabwe. Waangalizi wa uchaguzi kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (Sadc), wamekosoa mwenendo mzima wa uchaguzi nchini Zimbabwe ambapo kura zinaenendelea kuhesabiwa.
Sadc imesema upigaji kura ulikuwa wa amani, lakini baadhi ya vipengele havikufuata sheria na miongozo ya uchaguzi ya nchi hiyo.
Jumatano wiki hii zaidi ya wasimamizi 40 wa kura walikamatwa walipokuwa wakijaribu kujumuisha kura ambazo hazikupigwa na wananchi.
Kukamatwa kwa watu hao kumelaaniwa na makundi ya kutetea haki za binadamu.
Rais Emmerson Mnangagwa anawania kuchaguliwa tena kwa awamu ya pili huku ukosefu wa ajira na mfumuko wa bei vikitajwa kuwa kilio kikubwa nchini humo.
Mpinzani wake mkuu ni Nelson Chamisa wa chama cha Citizens Coalition for Change.