Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi 37 wateketezwa kwa moto na waasi Uganda

Lori la kivita la Jeshi la Uganda  UPDF likiwa limeegeshwa katika Shule ya Sekondari Lhubiriha katikati ya mji wa Mpondwe Wilaya ya Kasese Magharibi mwa Uganda ambapo wanafunzi waliuawa na wengine kadhaa kutekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa waasi.

Muktasari:

  • Mauaji hayo yametokea huku kukiwa na mashambulizi ambayo hayajawahi kushuhudiwa na wanajeshi wa Kongo na Uganda dhidi ya kundi la Islamic State.

Kundi la wapiganaji lenye mafungamano na Waasi wa Dola ya Kiislamu ‘Islamic State’ wamewaua wanafunzi 37 wa Shule ya Sekondari  Magharibi mwa Uganda kwa kuwateketeza kwa moto, Msemaji wa Jeshi la Uganda amethibitisha.

Kulingana na taarifa ya Jeshi la nchini hiyo, kundi la wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF) wanasakwa baada ya shambulio la kuvuka mpaka mwishoni mwa Ijumaa katika shule ya Sekondari Lhubiriha iliyopo  Mpondwe wilayani Kasese karibu na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wachunguzi wamesema, mabweni ya wanafunzi yalichomwa moto na wanafunzi kukatwa kwa visu katika shambulio la ADF usiku wa manane,

ADF linatajwa kuwa  moja ya makundi mabaya zaidi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Miili 37 imegunduliwa na kufikishwa katika chumba cha kuhifadhi maiti Hospitali ya Bwera," Msemaji wa Jeshi la Uganda (UPDF) Felix Kulayigye amesema.

Ameongeza kuwa “Watu wanane wamejeruhiwa huku wengine sita wakitekwa nyara na kuchukuliwa na washambuliaji kuelekea Mbuga ya Kitaifa ya Virunga, ambayo inapitia mpaka wa DR Congo, ameeleza.

Kulayigye amesema UPDF imeanza kuwasaka wahusika ili kuwaokoa wanafunzi waliotekwa nyara.

Kamishna Mkazi wa Kasese, Joe Walusimbi, aliambia AFP takriban 25 kati ya waliofariki wamethibitishwa ni wa shule hiyo.

Tukio hilo la mauaji ndilo shambulio baya zaidi kuwahi kutokea nchini Uganda, tangu milipuko miwili ya mabomu mjini Kampala mwaka 2010 kuwaua 76 katika shambulio lililodaiwa na kundi la Al-Shabaab lenye makao yake nchini Somalia.

Kwa mujibu wa AFP, Polisi na vitengo vya kijeshi nchini Uganda vilitahadharishwa kuhusu "shambulio kubwa" katika Shule ya Sekondari ya Lhubiriha huko Mpondwe saa 11:00 jioni siku ya Ijumaa.

Shule hiyo iliyofanyiwa shambulio ipo umbali wa kilomita mbili (maili 1.2)  kutoka mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo ADF inashiriki kikamilifu na imeshutumiwa kuua maelfu ya raia tangu 1990.

Kwa upande wake, Meja Jenerali Dick Olum aliambia shirika la AFP kuwa ADF ilikuwa eneo la tukio siku mbili kabla ya tukio.

Amesema kwa mazingira yaliyobainika, washambuliaji walikuwa na taarifa za kina kuhusu shule hiyo.

"Walijua mahali mabweni ya wavulana na wasichana yalipoishi," amesema Olum
Ameongeza kuwa "Ndio maana waasi walifunga bweni la wavulana na kulichoma moto. Waasi hawakufunga sehemu ya wasichana na wasichana walifanikiwa kutoka, lakini walikatwa kwa mapanga walipokuwa wakikimbia kwa usalama, na wengine kupigwa risasi".

Amesema baadhi ya miili hiyo, ilichomwa moto kiasi cha kutotambulika na uchunguzi wa DNA utahitajika ili kubaini miili hiyo.

"Tumetoa wito wa kuongeza nguvu kusaidia katika operesheni ya uokoaji wa waliotekwa nyara na kutafuta maficho ya waasi kwa ajili ya hatua za kijeshi," ameeleza.