Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanajeshi Gabon watangaza kuongoza nchi, wafunga mipaka

Gabon. Maofisa wa Jeshi la Gabon wametangaza kuiongoza nchi hiyo katika kituo cha televisheni cha Taifa hilo, ikiwa ni siku chache tangu Uchaguzi Mkuu ufanyike.

Pia wamesema wanafuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumamosi, ambapo Rais Ali Bongo alitangazwa mshindi.

Tume ya uchaguzi ilisema Bongo alishinda chini ya thuluthi mbili ya kura katika uchaguzi ambao upinzani ulidai kuwa ulikuwa wa udanganyifu.

Kupinduliwa kwa bongo kunatamatisha uongozi wa familia yake iliyodumu kwa miaka 53 madarakani nchini Gabon.

Wanajeshi 12 walionekana kwenye televisheni siku ya Jumatano, wakitangaza suala hilo huku pia wakitangaza kufunga mipaka ya nchi hiyo.

"Tumeamua kulinda amani kwa kukomesha utawala uliopo,"alisema mmoja wa wanajeshi hao.

Ofisa huyo wa jeshi aliongeza kuwa sababu nyingine ni; "utawala usiowajibika, usiotabirika na kusababisha kuzorota kwa uwiano wa kijamii ambao unahatarisha nchi katika machafuko".