Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ahadi ya Ndugai kwa wabunge wa Chadema

Muktasari:

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ameahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kwa wabunge 19 wa Viti Maalum Chadema walioapishwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo Jumanne Novemba 24, 2020.

Dar es Salaam. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ameahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kwa wabunge 19 wa Viti Maalum Chadema walioapishwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo Jumanne Novemba 24, 2020.

Akizungumza baada ya kuwaapisha wabunge hao, Ndugai ameeleza kuwa atawapa ushirikiano wote ili waweze kutimiza majukumu yao.

“Neno langu kwenu nendeni mkawatumikie  watanzania, naahidi kuwapa kila aina ya ushirikiano, najua kambi yenu itakuwa ya wabunge wachache wajibu wa spika ni kuwalinda walio wachache.”

“Nitajitahidi kuwalinda kuwapa haki  ili muweze kutekeleza majukumu yenu ya kuwatumikia Watanzania na muweze kufanya kazi yenu ya kikatiba kwa ukamilifu,” amesema Ndugai.