#LIVE: Rais Samia akizungumza na viongozi wa kisiasa

#LIVE: Rais Samia na viongozi wa kisiasa

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne, Januari 3, 2022 anakutana na viongozi wa vyama 19 venye usajili kamili wa siasa nchini humo.

Kikao hicho kinachofanyikiwa Ikulu jijini Dar es Salaam, kila chama kinawakilishwa na watu wanne, mwenyekiti, makamu wenyeviti wawili wa Bara na Zanzibar pamoja na katibu mkuu.

Miongoni mwa viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.

Mawaziri na viongozi mbalimbali wa Serikali nao ni sehemu ya kikao hicho wakiwemo, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Pia, kuna viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamoja na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).