Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madereva taksi mtandao watetewa

Muktasari:

  • Wakati biashara za mtandaoni zikiendelea kushika kasi na kuwa chanzo cha ajira kwa vijana nchini, imebainika kuwa sekta ya huduma za usafiri kwa mtandao haijali stahili za watendaji wake.

Dar es Salaam. Wakati biashara za mtandaoni zikiendelea kushika kasi na kuwa chanzo cha ajira kwa vijana nchini, imebainika kuwa sekta ya huduma za usafiri kwa mtandao haijali stahili za watendaji wake.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti, Sera na Uchumi (Repoa), uliohusisha kampuni sita za usafiri mtandaoni, madereva wengi wanaofanya kazi kwenye kampuni zinazotoa huduma za usafiri kwa njia ya mtandao hawana mikataba, hawalipwi vizuri na hawapati mahitaji muhimu, ikiwemo bima ya afya na fursa zilizopo kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo juzi, Dk Hilda Mwakatumbula alisema wamebaini kuwa madereva wanakandamizwa na wanalazimika kufanya kazi hiyo kwa sababu ya ugumu wa maisha.
“Tumebaini hakuna kampuni hata moja inayozingatia kigezo cha masharti nafuu kwa madereva,” alisema Dk Hilda.

Akizindua ripoti hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Ajira katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Joseph Nganga alisema Serikali itayachukua matokeo ya ripoti hiyo na kuyafanyia kazi katika utengenezaji wa sera na miongozo katika sekta hiyo, ambayo ni mpya na inatengeneza ajira nyingi.
Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Madereva wa Mtandaoni (Toda), Frank Mwezegule alisema matokeo ya utafiti huo ni uhalisia wa wanayopitia madereva hao. Alisema kubwa zaidi ikiwa ni changamoto ya mikataba na kukosa bima inayowafanya wasiwe na uhakika wa usalama wao.