Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mauaji ya Geita yafunga maduka, wafanyabiashara wahofu kukamatwa

Baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa katika eneo la Lulembela

Muktasari:

  • Wafanyabiashara wamepata hofu kufungua maduka kutokana na vurugu zilizoibuka jana baina ya wananchi na polisi na kusababisha watu wawili kufariki dunia.

Mbogwe. Eneo la Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita asubuhi ya leo Alhamisi Septemba 12, 2024 hadi sasa (Saa 4:10 asubuhi) wafanyabiashara hawajafungua maduka wakidai kuhofia kukamatwa na polisi.

Chanzo cha hofu hiyo ni vurugu zilitokea jana baina ya wananchi na polisi na kusababisha watu wawili kuuawa huku kituo cha polisi kikishambuliwa kwa mawe.

Baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa katika eneo la Lulembela

Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi jana Jumatano, David Misime imesema katika vurugu hizo waliopoteza maisha ni mwanaume mmoja ambaye jina lake halijafahamika anayekadiriwa kuwa na miaka 18 -20 na mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Lulembela, Theresia John (18). 

Mwananchi Digital imefika eneo la tukio na kushuhudia maduka zaidi za 50 katika eneo hilo yamefungwa.

Baadhi ya wananchi ambao wameogopa kutaja majina yao wakihofia kukamatwa na polisi wamesema kutokana na vurugu zilizotokea jana wafanyabiashara wana hofu.

"Hapa siyo maduka tu hata nyumbani vijana wameondoka wanaogopa, wanaume nao hawapo kila mmoja anahofia kukamatwa, kama hivi tunashindwa kupata huduma maduka yamefungwa, bodaboda hazifanyi kazi kwa kweli ni mateso," amesema mmoja ya wakazi wa eneo hilo kwa sharti la kutotajwa jina wala kupigwa picha.

Kituo cha Polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita

Hata hivyo, Ofisa Mtendaji Kata ya Lulembela, Frank Gonyo amesema hawajazuia wafanyabishara kufungua maduka lakini hali iliyopo sasa imetokana na hofu baada ya vurugu zilizotokea jana.

Katika taarifa ya jana, Misime amesema chanzo cha vurugu hizo ni baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa kwenye mnada wa Lulembelea kuwadhania kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambulia.

Gari lililochomwa na wananchi nje ya Kituo cha Polisi Lulembela.

“Walipokuwa wanawashambulia alitokea ofisa mtendaji wa kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Lulembela. Hata hivyo, wananchi wanaokadiriwa takribani 800 walifika kituoni na kuwataka polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue," amesema Misime kwenye taarifa yake.