Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Ramadhan itumike kuliombea Taifa’

Shekhe wa Mkoa wa Mbeya, Ayasi Njalambaa (wa kwanza kulia) akichukua futari iliyoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust ambayo Mkurugenzi wake ni Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson (katika) ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Sheikh wa Mkoa wa Mbeya, Msafiri Njalambaha ametaka mwezi mtukufu wa Ramadhan utumike kuliombea dua Taifa na kukemea vitendo viovu dhidi ya watoto.

Mbeya. Sheikh wa Mkoa wa Mbeya, Msafiri Njalambaha amekemea vitendo vya kikatili vinavyoendelea nchini na kuomba waumini wa dini ya Kiislamu kutumia mwezi mtukufu wa Ramadhan kuliombea Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Njalambaha ameyasema hayo usiku wa jana Jumatatu Aprili  17, 2023 wakati wa futari iliyoandaliwa na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kupitia Taasisi ya Tulia Trust iliyohusisha  waumini wa dini ya Kiislamu, viongozi wa Serikali na wadau zaidi ya 1,000 walioshiriki.

“Vitendo viovu vya utatili wa kijinsia, ulawiti, na watu kujinyonga vinatokana na jamii kukosa mafundisho ya Mungu na kwenda kinyume umefika wakati viongozi wa dini kutoa elimu ili waweze kurejesha kwenya imani za dini na kujua vitabu vinasema nini katika kumcha Mungu,” amesema.

Ameshukuru Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kwa kuwakusanya waumini wa dini hiyo kupitia taasisi yake jijini humo ikiwa ni mara ya saba mfululizo.

Akizungumza kwa niaba ya Dk Tulia, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amesema kama viongozi wa Serikali wataendelea kuungana na waumini wa dini ya Kiislamu katika mfungo wa kuelekea sikukuu ya Eid el Fitr.

“Tunayaona haya yanayofanywa na kiongozi huyu wa Bunge kwa kweli ni mambo ya kujivunia kupitia taasisi yake ya Tulia Trust, ambapo siku ya Ramadhani wanatarajia kusashika mkono watoto 200 wanaoishi katika mazingira magumu na yatima mkoani hapa,” amesema Malisa.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Dourmohamed Issa amesema ni wakati sasa waumini wa dini hiyo kuungana na kushirikiana na Serikali katika kuliombea Taifa la Tanzania na Mbunge wa Mbeya mjini kwani amekuwa hana ubaguzi kwa kuwatumikia watu wote.

“Kupitia adhara hii twapaswa kuungana na Serikali yetu kumuombe Rais Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson na viongozi wengine wakuu wa nchi kwani tunaona jinsi Mkoa wa Mbeya unavyopiga hatua za maendeleo katika nyanja mbalimbali,” amesema.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sabasaba, Ally Mbika amesema jamii ikiwa mstari wa mbele kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo itaitengenezea njia Serikali kuchukua hatua kwa walengwa wanaochochea vitendo hivyo.