Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yajipanga kuutokomeza ukoma

Muktasari:

Imesema takwimu zinaonyesha Tanzania imepiga hatua katika kutokomeza ugonjwa huo kutokana na kiwango cha watu wanaougua kupungua mara mbili katika kipindi cha miaka tisa.

Dar es Salaam. Wizara ya Afya imesema licha ya kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti ugonjwa wa ukoma, bado juhudi zinahitajika kuhakikisha unatokomezwa nchini.

Imesema takwimu zinaonyesha Tanzania imepiga hatua katika kutokomeza ugonjwa huo kutokana na kiwango cha watu wanaougua kupungua mara mbili katika kipindi cha miaka tisa.

Takwimu hizo zilitolewa juzi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika kuelekea siku ya ukoma duniani ambayo huadhimishwa kila Jumapili ya mwisho ya Januari, ambayo kidunia inaadhimishwa leo.

Mwalimu alisema takwimu zinaonyesha kupungua kwa ugonjwa kutoka watu 0.9 kati ya watu 10,000 mwaka 2006 hadi kufikia watu 0.4 kati ya 10,000 mwaka 2015.

Alisema takwimu hizo zinaonyesha katika kila Watanzania 10,000 kiwango cha watu wenye ugonjwa wa ukoma sasa ni watu 0.4.

Kwa habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi