Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Tumieni sayansi kugeuza changamoto kuwa fursa’

Muktasari:

Wanafunzi wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari nchini wametakiwa kuongeza juhudi katika kujikita kwenye bunifu zinazogeuza changamoto za jamii kuwa fursa.

Dar es Salaam. Wanafunzi wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari nchini wametakiwa kuongeza juhudi katika kujikita kwenye bunifu zinazogeuza changamoto za jamii kuwa fursa.

Hatua hiyo ya kubadilisha changamoto kuwa fursa itachangia kwa kiasi kikubwa kusaidia jamii na kupunguza kilio cha vijana nchini.

Wito huo umetolewa Desemba 16, 2022 na Mkurugenzi wa Huduma wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Emmanuel Mgonja wakati wa kufunga mafunzo ya miezi 10 ya wanafunzi wa sekondari yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema mafunzo hayo yatasaidia kubadilisha mitazamo ya kifikra miongoni mwa vijana kuhusu sayansi na badala yake kutumia masomo hayo kama fursa ya kibiashara katika kutatua changamoto katika jamii.

Mgonja amesema, “Niwaombe wanafunzi wa masomo ya sayansi Kuongeza juhudi katika kujikita kwenye bunifu zinazolenga kutataua matatizo yanayozunguka katika jamii

“Haya ni mafunzo muhimu na mazuri ambayo yatachochea vijana wengi kuona sayansi ni fursa inayosaidia si tu kutoa majibu ya maswali yanayotusumbua bali pia kutengeneza ajira,” amesema.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBI), Dk Erasto Mlyuka amesema taasisi hiyo inalenga kuhakikisha bunifu zinakuwa na kuzipeleka sokoni.

 “DTBI tumekuja na model ambayo inashirisha patners ambao ni watekelezaji upande wa sayansi ikiwemo wabunifu, waalimu na bussiness mentors ambapo anaamini kupitia ushirishwaji huo taifa litakwenda kupiga hatua katika maendeleo ya kiteknolojia.

 “Tupo katika hatua ya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa nchi nzima ili kuwafikia wabunifu wengi na kutoa hamasa kwa vijana kusoma masomo ya sayansi,” amesema Dk Mlyuka