Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Ugonjwa wa surua unaweza kumpata mtu yeyote’

Baadhi ya Wahudumu wa Afya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani wakipita nyumba Kwa nyumba kuchoma chanjo ya Surua na Rubella baada ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Emmanuel Mwaigobeko kutangaza mlipuko wa ugonjwa huo jana. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Kufuatia kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa surua na rubella katika Manispaa ya Mtwara Mikindani zoezi la chanjo laanza kutolewa ili kuweza kukinga watoto chini ya miaka mitano na ugonjwa huo.

Mtwara. Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Lusungu Mselela  amekiri kuwepo kwa mlipuko huo ambapo alisema taarifa iliyopo sasa ni wagonjwa 14 wameshabaini baada ya sampuli zao kupimwa.

Akizungumza na Mwananchi alisema kuwa kitendo cha kupatikana wagonjwa zaidi ya watano katika eneo moja kwa tafsiri huo ni mlipuko kwa sasa tuko katika hatua za kudhibti kwa kutumia chanjo za magonjwa hao ambapo mpaka sasa surua (6) rubella (8).

“Magonjwa haya yanazuiliwa kwa kutumia chanjo na mwaka jana kuna watoto hawakufikiwa na huduma ya chanjo wamebainishwa na tumeanza kutoa chanzo ambapo ni kati ya umri wa mieizi 9-18 tunawatafuta na tumeamua kuwaita wote ili kuweza kuhakikiwa ili kujua nani alikosa chanjo,” amesema.

“Hapo kuna matatizo mawili wapo watoto walipata chanjo moja lakini ya pili hatawakupa lakini pia wapo ambao hawajapata kabisa hizo chanjo,”amesema.

“Homa ambazo haziishi mafua kikohozi macho kuwa na majimaji au mekungu na dalili ya wazi kabisa vipele kuanzia usoni  hatimae mwili,” amesema.

 “Kwa hatua hiyo tunawashauri wazazi na walezi wanatakiwa kuwapeleka watoto kwenye vituo vya kutolea huduma za chanjo vilivyopo  karibu na zahanati na vituo vya afya ili wakapate chanjo hiyo,” amesema.

“Ugonjwa huo wa surua unaweza kumpata mtu yeyote ukiona dalili uwepo wa vipele vidoogo vinavyoambatana na homa kali wahi kituo cha afya ili uweze kupata matibabu,” amesisitiza.


Kwa upande wake Mganga Mkuu Mkoa wa Mtwara, Hamad Nyembea  amesema kuwa mlipuko upo lakini ni mdogo ambao hata visa vimeongezeka mwezi wa pili wapo watoto walionekana kuumwa

 “Tukalazimika kupeleka sampuli na kwenda kuziangalia ambapo ilibainika kuwa wanaumwa ugonjwa,” amesema Dk Nyembea.

Naye Fatuma Said Mkazi wa Naliendele amesema kuwa ni vema watoto wakapatiwa chanjo hizo ili kuwakinga na magonjwa hayo.

“Mimi huwa nikisikia chanjo naenda zahanati kuuliza, nikishaeleweshwa na napeleka mtoto ili wapate chanjo kwakuwa naamini kuwa chanjo ni njia salama ya kudhibiti maambukizi dhidi ya magonjwa mbalimbali yakiwemo hayo,” alisema Said.