Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Watanzania tembeleeni makumbusho za Taifa’

Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah kairuki (katikati) akipata maelekezo kwa Mkurugenzi wa Makumbusho na nyumba za utamaduni, Adelaide Selema (kulia) wakati wa ziara yake aliyofanya katika makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salam.

Muktasari:

  • Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki na Naibu wake watembelea, Dustan Kitandula watembelea Makumbusho ya Taifa ya Posta watoa wito kwa Watanzania kujenga utaratibu wa kutembelea maeneo hayo ili kujifunza urithi na historia ya Tanzania.

Dar es Salaam. Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wamewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea makumbusho za Taifa ili kujifunza na kujua historia ya Tanzania ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Viongozi hao ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki na Naibu Waziri, Dustan Kitandula ambapo wametoa wito huo leo Ijumaa Septemba 22, 2023 walipotembelea Makumbusho ya Taifa iliyopo Posta jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari Kitandula amesema makumbusho ya Taifa yana utajiri mkubwa kwa Tanzania kwa kuwa yamehifadhi mambo kutoka maeneo tofauti hivyo ni vema watu wakatembelea ili kujifunza.

"Ni vema Watanzania wakapata fursa ya kuona na kujifunza, sisi tumetumia muda mwingi hapa (Makumbusho ya Taifa) kujifunza tulipokuwa kabla ya Uhuru na baada.Tumejifunza chimbuko la binadamu, Watanzania wawe na utamaduni kutembelea makumbusho.
"Tupo kwenye shughuli za kutembelea taasisi za wizara na kuona shughuli wanazozitekeleza, mikakati, mafanikio na  mchangamoto wanazokabiliana nazo. Tumekuja pia kuona na mila tamaduni za makusanyo yanayohifadhiwa," amesema Kitandula.

Naye,  Waziri Kairuki amesema wanatembelea taasisi za chini ya wizara hiyo kujitambulisha kwa watendaji na watumishi.
"Tunawakaribisha wanafunzi,  Watanzania wote na wageni kutembelea Makumbusho na kujifunza  historia ya kale kuanzia soko la watumwa na mambo mengine mengi.Kuna utalii na utajiri mkubwa katika Makumbusho ya Taifa," amesema Kairuki.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Noel Luoga amesema maboresho ya sheria ya mambo ya kale makumbusho ya Taifa hivi sasa yanaruhusu kuanzishwa kwa makumbusho binafsi.
Amesema wanaohitaji wanatakiwa kufuata taratibu mbalimbali zitakazoanishwa