Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto 400,000 kuchanjwa Manyara

Mratibu wa chanjo Mkoa wa Manyara, Seleman Manoza akizungumza na waandishi wa habari mjini Babati. Picha na Joseph Lyimo

Muktasari:

Watoto wenye umri wa miaka mitano wa Mkoa wa Manyara, wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa polio kuanzia Desemba mosi hadi 4, 2022.

Babati. Watoto 400,000 walio chini ya miaka mitano katika Mkoa wa Manyara wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa polio.

  

Chanjo hiyo ni kwa ajili ya kuwakinga na ugonjwa wa polio ambao unaweza kusababisha maradhi mbalimbali ikiwamo ulemavu pamoja na vifo.


Ofisa afya Mkoa wa Manyara, Sultan Mwabulambo ameyasema hayo mjini Babati leo Jumanne Novemba 29 wakati akizungumza na Mwananchi.


Mwabulambo amesema chanjo hiyo itaanza Disemba mosi hadi 4 mwaka huu na kutolewa kwenye wilaya zote tano za mkoa huo.


Amesema wataalamu watapita nyumba kwa nyumba, shuleni na katika maeneo yenye mikusanyiko ili kuwafikia watoto wenye umri chini ya miaka mitano.


Mratibu wa chanjo mkoa wa Manyara, Seleman Manoza amesema chanjo hiyo ni muhimu kwa watoto ili kuwanusuru na magonjwa mbalimbali.


Manoza amesema wazazi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa wataalamu wa afya pindi wanapofika katika maeneo yao.


Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Dk Aristidy Raphael amesema wamejipanga kuhakikisha watoto chini ya miaka mitano wanapata chanjo hiyo.