Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

13 wahofiwa kupoteza maisha mitumbwi miwili ikizama Ziwa Victoria

Muktasari:

Mwili wa mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja umeopolewa kutoka Ziwa Victoria huku watu wengine 13 wakihofiwa kufa maji na wengine 14 kuokolewa baada ya mitumbwi miwili kuzama ndani ya ziwa hilo wakati wakitoka kanisani.

Musoma. Watu 13 wanahofiwa kufariki dunia huku wengine 14 wakiokolewa baada ya mitumbwi miwili kuzama ndani ya Ziwa Victoria wakati wakitoka kusali ibada ya Jumapili Kijiji cha Ichigondo Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi leo Jumatatu Julai 31, 2023, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano amesema tukio hilo lilitokea jana saa 12:30 jioni na tayari mwili wa mtoto anayekadiriwa kuwa na mwaka mmoja umeopolewa. 

“Hapa Kijiji cha Igundu kuna kama ras sasa watu walikuwa wakitoka kusali katika kanisa la KTMK  ndipo mtumbwi mmoja ukapigwa na dhoruba na kuanza kuzama, ukaja mtumbwi wa pili kwaajili ya kuokoa nao ukapigwa na dhoruba mitumbwi yote miwili ikazama,"amesema Dk Naano

Dk Naano amesema jitihada za kuwatafuta watu hao 13 zinaendelea akidai jana baada ya giza kuingia zoezi la kuwatafuta lilisitishwa.

"Tupo hapa na timu ya usalama ya wilaya tunaendelea kuwatafuta maana jana baada ya giza kuingia hakuna ambacho kingeweza kufanyika ila tu hadi sasa ni mwili mmoja ndio umeopolewa,” amesema

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agostino Magere amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.

“Ndio nimepokea hizo taarifa na hapa ninajiandaa nielekee huko nadhani nitakuwa kwenye nafasi nzuri kulizungmzia nikishafika eneo la tukio,”amesema Magere