Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

25 wakimbizwa hospitali wakidaiwa kunywa pombe yenye sumu Songwe

Muktasari:

  • Watu 31 wadaiwa kunywa pombe yenye sumu huku kati yao 25 wakikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi kwa matibabu

Songwe. Taharuki imeibuka katika Kijiji cha Halambo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe baada ya watu 25 kufikishwa katika hospitali ya wilaya hiyo kwa madai ya kuugua baada ya kunywa pombe ya kienyeji.

Inadaiwa watu hao walikunywa pombe hiyo sehemu moja ambapo baadae walianza kuumwa tumbo na kuhara na walipatiwa huduma ya kwanza katika zahanati ya kijiji hicho.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Halambo, Lazima Mwambani amesema siku ya tukio hilo Ijumaa Juni 2, 2023 kulikuwa na msiba kijijini hapo ambapo baada ya mazishi watu walienda kunywa pombe kilabuni hapo.

"Tukio hilo lilitokea Juni 2 mwaka huu na idadi ya walioathirika ni watu 31 ambapo baadhi yao walipata madhara siku hiyohiyo lakini wengine walianza kuumwa siku iliyofuata" amesema Mwambani.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Dk Nelson Mponjoli amesema aliwapokea watu 25 ambao walitibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani kwao.

"Siwezi kuthibitisha kama walikunywa kinywaji chenye sumu ninachoweza kusema watu 25 walifikishwa hospitalini wakiwa wanasumbiliwa na kuhara na tumbo kuuma, hata hivyo hali zao hazikuwa mbaya walitibiwa na kuruhusiwa kurudi," amesema Mponjoli

Aidha, Mwenyekiti wa kijiji hicho amesema mpishi wa pombe hiyo anadaiwa kukimbia mara baada ya kusikia watu wanaumwa, lakini mume wake anashikiliwa na Polisi.

Pia, kati ya watu 31 waliokumbwa na madhara hayo inasemekana 25 tu ndio waliofikishwa hospitali ya wilaya huku wengine sita wakitibiwa sehemu nyingine.