Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

64 mbaroni Dodoma, wamo 29 wakituhumiwa utapeli ajira za Q Net

Kamanda Polisi Mkoa wa Dodoma, Gallus Hyera akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma. Picha na Elidaima Mangela

Muktasari:

  • Watuhumiwa hukusanya fedha kwa wananchi kwa kigezo cha kuwapatia fursa za ajira ndani na nje ya nchi.

Dodoma. Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu 64 wakiwemo 29 wanaotuhumiwa kujihusisha na utapeli kupitia mtandao wa Q Net.

Watuhumiwa hao 29, wamekuwa wakikusanya fedha kutoka kwa wananchi katika maeneo ya jiji hilo kwa ahadi ya kuwapatia fursa za ajira ndani na nje ya nchi.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gallus Hyera, Jijini Dodoma wakati akizungumza na vyombo vya habari, ambapo amesema watuhumiwa wamemkamatwa kufuatia msako na oparesheni kati ya Juni 8 hadi Julai 5, 2026.

Kamanda amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kuwahamasisha watu kutoa fedha kwa madai ya kuwapatia fursa za ajira ndani na nje ya nchi ahadi ambazo hazikutekelezwa.

“Tumekamata watuhumiwa 29 wanaotumia mtandao wa Q Net kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu kwa kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa kigezo cha kuwapatia fursa za ajira ndani na nje ya nchi,” amesema Hyera.

Amesema uchunguzi wa awali unaendelea ili kubaini ukubwa wa mtandao huo, idadi ya waathirika na kiasi cha fedha kinachodaiwa kupotea kupitia utapeli huo na watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Mbali na hao, Jeshi hilo pia linawashikilia watu 31 kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi kilo 12, mirungi kilo 6, mtambo mmoja wa kutengenezea pombe ya moshi na pea moja ya sare ya Jeshi.

Miongoni mwa watuhumiwa hao 31, wapo wanatuhumiwa wa wizi wa pikipiki na televisheni ambapo mpaka kufikia sasa wamekamatwa na pikikipi tano aina ya haojue, boxer na televisheni mbili.

Hyera amesema watuhumiwa hao pia wamekutwa na vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji 49, vipande 8 vya alluminium na vipande 19 vya nondo, ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha vilikuwa vya wizi na vilikusanywa kutoka maeneo tofauti ya Jiji hilo.

Kuhusu wizi wa pikipiki, amesema Jeshi hilo linawashikiliwa watuhumiwa wanne wakazi wa Kibaigwa jijini humo kwa tuhuma za kuiba pikipiki katika maeneo tofauti ya ndani ya Mkoa huo kisha kuzisafirisha Mikoa mingine ili kuziuza au kuzitumia kwa shughuli zao.

“Kwa upande wa wizi wa pikikipiki tunawashikilia watuhumiwa wane wakazi wa Kibaigwa kwa tuhuma za kuiba pikipiki hapa Mkonia kisha kuzisafirsha nje kwa ajili ya kuziuza,” amesema Hyera.

Amesema Jeshi hilo kupitia kikosi cha usalama barabarani limewafungia leseni madereva saba kwa muda wa miezi mitatu kwa makosa ya ajali kupita vyombo vya usafiri ikiwemo makosa ya mwendokasi na kuzidisha abiria.

Aidha Hyera amewataka wananchi kuwa makini na ahadi za ajira zinazotolewa na watu au mitandao isiyo, kutafuta uthibitisho na kuwa na utaratibu wa kuhakiki taarifa kabla ya kutoa fedha.

Amewaasa pia wananchi kujitafutia pesa kwa njia ya halali na kufuata sheria za nchi na kushirikiana na Jeshi la polisi kwa kutoa taarifa juu ya watu wasiofaa katika jamii ili wadhibitiwe kabla ya kuleta madhara.