Wanne mbaroni Mtwara kwa tuhuma za uhalifu wa kimtandao
Watuhumiwa wanne wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya utapeli na uhalifu wa kimtandao katika mikoa 11 nchini.
Muktasari:
- Watuhumiwa wanne wanaodaiwa kuendesha mtandao wa utapeli wa kimtandao katika mikoa 11 nchini wamekamatwa mkoani Mtwara, wakiwa na simu 10 na laini zisizosaji-liwa kwa majina yao halisi
Mtwara. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara kupitia Kitengo cha Makosa ya Kimtandao limewakamata watuhumiwa wanne wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya utapeli na uhalifu wa kimtandao katika mikoa 11 nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi, Julai 4, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Issa Suleiman amesema watuhumiwa hao wameku-wa wakifika Mtwara kwa nyakati tofauti kufanya matukio ya utapeli dhidi ya watoa huduma za kifedha ka-bla ya kuondoka kuelekea maeneo mengine.
Watuhumiwa waliokamatwa ni Ibra-himu Mfinanga maarufu DJ Ibra (27), Steven Matiko maarufu Kurya Boy (29), George Angima (30) na Danie Marwa (20), wote wakazi wa Mkoa wa Mwanza.
Kamanda Suleiman amesema uchun-guzi wa awali umebaini kuwa wa-tuhumiwa hao wamehusika na matukio ya uhalifu wa kimtandao katika mikoa ya Iringa, Tanga, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Mbeya, Dodoma, Pwani, Shinyanga na Mwanza.
Amesema wakati wa kukamatwa kwao, Polisi walikuta simu 10 pamoja na laini 10 za mitandao mbalimbali ambazo hazikuwa zimesajiliwa kwa majina yao halisi zinazodaiwa kutumi-ka katika kutekeleza vitendo hivyo vya kihalifu.
“Watuhumiwa hawa walikuwa wakifi-ka kwa mawakala wa huduma za kifedha wakijifanya wateja wa kawai-da, kisha kuomba kutumia simu zi-nazotumika kufanya miamala na kuhifadhi namba hizo kwa majina ya mitandao husika kwa ajili ya kuende-leza uhalifu wao,” amesema Kamanda Suleiman.
Ameeleza kuwa, uchunguzi wa tukio hilo unaendelea sambamba na jitihada za kuwabaini washirika wengine wa watuhumiwa hao na kwamba baada ya kukamilika kwa uchunguzi watafi-kishwa kwenye mamlaka za kisheria.
Aidha, wananchi ambao ni waathirika wa matukio hayo ndani ya Wilaya ya Mtwara wametakiwa kufika Kituo Kikuu cha Polisi Mtwara kwa ajili ya kuwatambua watuhumiwa hao na ku-saidia kukamilisha uchunguzi.
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limetoa wito kwa mawa-kala wa huduma za kifedha kuepuka kutoa simu wanazotumia kufanya mi-amala kwa watu wasiowafahamu ili kuzuia kutoa mwanya kwa wahalifu kutekeleza uhalifu wa kimtandao.